Thursday, December 8, 2016

U-HEARD-: POVU LA Q CHIEF BAADA YA NGOMA YAKE ALIYOMSHIRIKISHA PATORANKING KUVUJISHWA

Kwa bahati mbaya imeingia mtaani ngoma ya msanii wa Bongo Fleva Q Chief kwa kinachosemekana kuwa imevujishwa na producer wa awali ambaye aliiandaa kazi hiyo.
Amesikika Q Chief kwenye U-Heard katika kipindi XXL ya Clouds Fm leo hii akionyesha kuwa mwenye masikitiko makubwa kutokana na tukio hilo. Kwa madai yake Q Chief amedai kuwa mipango yake ilikuwa ni kuiachia ngoma hiyo mwezi january mwakani kama Mungu angetia baraka zake.
Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba ngoma hiyo ambayo imevuja sio original version, hiyo ni Demo, na Q Chief ametoa maombi kwa wapenzi wote wa muziki mzuri na media tofauti tofauti kuto ipiga ngoma hiyo kwasababu haina viwango kabisa kulinganisha na original version na hivyo kudai kuwa atatoa muongozo ni lini ataiachia ngoma hiyo rasmi.
Unaweza kumsikiliza hapa Q Chief wakati akitoa Povu hilo kwenye U-Heard ya leo December 8 kwa kuplay hii video hapa chini

0 maoni:

Post a Comment