Wednesday, December 14, 2016

MZIWANDA ANENA HAYA KWA MKE WAKE MPYA#johnleo

Wahenga wanasema “kila m-bamba ngoma huvutia upande wake”  msemo huo hauna utofauti mkubwa sana na msimamo wa msanii wa Bongo FLeva hitmaker wa ngoma ya Jike Shupa Nuh Mziwanda.
Ni baada ya kufunguka kwenye kipaza chaPerfect255 kuwa anamuona mke wake bibieNawal kuwa ndiye mwanamke wake bora kabisa kati ya wote ambao amewahi kuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi.
Mziwanda ametolea ufafanuzi kauli yake hiyo na kudai kuwa ubora wa mwanamke huyo unakuja pale anapokuwa anajali kazi yake bila kuweka wivu mbele na vitu kama hivyo.
“Mwanamke wangu anajua kunitreat vizuri, mpole, mstaarabu, ananisikiliza, ananiachia nifanye kazi tofauti na zamani ambapo nilikuwa nikienda kwenye show lazima unikute na bodyguard pembeni.”
Hayo ni baadhi tu ya maneno na sifa ambazo Nuh Mziwanda amemmwagia baby mama wake Nawal. Kusikiliza full interview bonyeza play kwenye hii video hapa chini.

0 maoni:

Post a Comment