Mheshimiwa Mwigulu NCHEMBA (wewe ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi)..,
.., leo asubuhi ulikuwa katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na kituo cha matangazo cha Star TV.., nimekusikia kauli zako, kuhusu 'issue' ya watu wale 7 waliokutwa mto Ruvu wakiwa wamekufa (vifo vya ajabu), umesema kwamba watu wale ni WAHAMIAJI HARAMU .., mimi nikuulize maswali yafuatayo;
(i) Je, wahamiaji haramu ndiyo wanapaswa kuuwawa na kutupwa mto Ruvu!?
(ii) wahamiaji haramu ndiyo wanapaswa kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali na kuuawa!?
(iii) wahamiaji haramu ndiyo wanatakiwa kuuwawa na kufungwa kwenye mifuko ya Sandarusi na kuwekwa mawe ndani!?
(iv) sheria za nchi, sheria za jeshi la polisi, sheria za idara ya uhamiaji zinasema nini kuhusu wahamiaji haramu.., kuuwawa!?
(v) kama kweli ni wahamiaji haramu.., nani ametoa idhini ya kuwaua, nani amewaua, na kwanini watupwe mto Ruvu wakiwa wamefungwa kwenye mifuko na mawe ndani yake!?
.., niendelee kukuliza mheshimiwa waziri.., hao wahamiaji haramu, wanatoka katika nchi gani.., Je, nchi zao zikigundua kwamba mliwaua watu wao na kuwazika huko Bagamoyo, hauoni mnaleta mgogoro mkubwa wa kidiplomasia!?
Mheshimiwa waziri, kazi ya jeshi la polisi ni kulinda watu na mali zao, kuhakikisha usalama wa raia ni kiwango cha juu, bila kuhatarisha usalama wao, maana wao ndiyo kipaumbele cha kwanza cha serikali (walipa kodi)..,
.., umetoa ufafanuzi hafifu sana kuhusu suala la kupotea kwa Ben Saanane na kutoonekana kwa kitambo kirefu.., kuna maswali ya kuoanisha hapa;
(i) kwanini ile miili 7 iliyokutwa kule Ruvu izikwe kwa haraka ile na halmashauri!?
(ii) kwanini jeshi la polisi, halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo hawakutaka kufanya uchunguzi kubaini nini chanzo!?
(iii) kwanini jeshi la polisi liko kimya hadi sasa, wiki nzima, hadi 'pressure' ya watanzania inakuibua wewe waziri, tena kwa kuulizwa!?
(iv) Je, wakati huu ndugu, jamaa, rafiki wa Ben Saanane wakiwa katika sintofahamu ya ndugu yao, kwanini Jeshi la polisi halikuona umuhimu wa kutokuzika maiti zile kwa haraka ile!?
(v) kuna kila sababu ya kumtaka OCD wa Bagamoyo na vyombo vya ulinzi na usalama katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, kutoa kauli yenye kueleweka.., (wako chini ya ofisi yako hawa watu)
NB; Pia.., kuna habari moja iliwahi kutangazwa na ITV mwezi wa August, mwaka 2016, naomba kunukuu sehemu ya habari ile..,
".., Zaidi ya watanzania 56 katika vijiji vya Chamchuzi na Buguluka vilivyoko katika kata ya Bwelanyange iliyoko wilayani Karagwe mkoani Kagera waliokuwa wakijihusisha na shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera na ziwa hiema wanadaiwa kutekwa na kuuawa kikatili na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani Rwanda ambao mara kwa mara hufanya doria ndani ya mto huo na ziwa hilo. "
.., kitu cha kusikitisha sana.., serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi.., haikuwahi kutoa kauli, taarifa yoyote juu ya habari hiyo.., mbaya sana!
Mwisho ;
Jeshi la polisi kupitia intelejensia yake, wanapaswa kuwa 'proactive' kuliko kuwa 'reactive' kwenye masuala ya ulinzi wa mali za umma na usalama wa raia.., intelejensia ya jeshi la polisi inatakiwa kufanya kazi kubwa kabla umma kupiga kelele ndiyo wao wachukue hatua.., (kama jeshi la polisi linaweza kubaini kuhusu vurugu kutokea katika mkutano wa kisiasa ambao haujafanyika.., linashindwa nini kubaini usalama wa raia na mali zao!?)
matukio ya watanzania kuuwawa yamekuwa yakiongezeka kila kunapokucha, watanzania 9 katika wilaya ya Kyelwa waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera waliuwawa na watu wanaodhaniwa askari wa nchi jirani ya Rwanda hali ambayo ilikusikitisha wewe (waziriwa mambo ya ndani) wakati huo ukiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Kagera.., (lakini wizara yako haikutaka kutoka mbele ya watanzania na kusema kitu, kuhusu matukio hayo)
Jeshi la polisi linapawa kuwa jeshi la kulinda raia na mali zao.., siyo jeshi la kulinda maslahi ya watu wachache sana katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania.., tazama, raia wanakufa vifo vya ajabu katika nchi yao, zinatoka kauli rahisi, kwamba ni wahamiaji haramu.., siyo sahihi.., tunapaswa kupata ukweli dhidi ya maiti zile zilzokutwa katika mto Ruvu.., pia tuelezwe;
(i) kwanini zitupwe mto Ruvu.
(ii) kwanini zifungwe na mawe ndani.
(iii) kwanini zifungwe katika mifuko ya Sandarusi.
(iv) kwanini zionekane kujeruhiwa na vitu vyenye ncha kali.
(v) kwanini mamlaka za usalama ziko kimya..,
Ahsante,
Mwananchi wa kawaida,
Martin Maranja Masese (MMM)
0 maoni:
Post a Comment