Friday, December 16, 2016

News: RAISI MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA DR MWELE#johnleo

Taarifa kutoka IKULU inasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 16 Desemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)Dkt. Mwele Malecela.
Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMRatakayejaza nafasi iliyoachwa wazi naDkt. Mwele Malecela utatangazwa baadaye.
December 15 2016 Dr. Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari Tanzania akizungumza kuhusu uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya leo.

FULL VIDEO: Wizara ya Afya yatoa tamko kuhusu ZIKA, bonyeza play hapa chini kupata taarifa kamili

0 maoni:

Post a Comment