Wednesday, December 14, 2016

CHAMA CHA CUF CHAGOMBANISH WANACHAMA WAKE#johnleo

December 14 2016 mahakama kuu ya Tanzania imesikiliza kesi iliyofunguliwa na Bodi ya wadhamini CUF dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama 11 wa chama hicho.
Kwenye kesi hiyo leo jaji wa mahakama kuu ya Tanzania, Sakieti Kihiyo anayesikiliza kesi hiyo amekataa ombi la bodi ya wadhamini CUF kuwa ajitoe kwenye kesi. Jaji Kihiyo amesema hawezi kujitoa kusikiliza kesi kwa kuwa hoja zao hazina msingi.
Baada ya maamuzi hayo nje ya mahakama kuu kumeibuka vurugu baina ya pande mbili zinazotofautiana za Wanachama wa CUF.
Awali Kesi hiyo iliposikilizwa December 6 2016 wakili wa bodi ya wadhamini CUF, Juma Nassoro aliomba Jaji anayesimamia kesi, Jaji Kihiyo ajiondoe kwenye kesi hiyo.
Wakili Nassoro alitaja hoja kuu mbili, ya kwanza alisema inajengwa na kesi hiyo wakati ilipotajwa Novemba 11, mwaka huu ambapo Jaji Kihiyo aliibua hoja iliyohusu uhalali wa wadhamini ambayo ilikuwa na muelekeo wa kuwaonyesha wadaiwa nini wafanye. Aidha hoja nyingine ni kauli iliyotolewa na Jaji huyo kwamba shauri hilo limefunguliwa kwa haraka haraka.
  • Lllll

0 maoni:

Post a Comment