Wednesday, December 14, 2016

BAHATI BUKUKU ASEMA HAYA BAADA YA KUZUSHIWA KIFO#johnleo


Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku ambaye hivi karibuni amezushiwa kufariki dunia kwa ajali, amekanusha taarifa hizo na kusema zimeandaliwa na watu wanaotaka kumpunguzia mashabiki.


Bahati Bukuku

Akizungumza na East Africa Television Bahati Bukuku amesema taarifa za kifo chake ni mbingu tu ndiyo zitajua, kwa kuwa shetani hana nafasi ya kujua taarifa za kifo chake.
"Ni watu ambao wanaamini wakiongea hivyo watanipunguzia mashabiki, mpango aliouandaa shetani hauwezi fanikiwa, kwa sababu kifo changu shetani hatatangulia kujua ila Mbingu zitajua, shetani hana sababu za kujua taarifa zangu", alisema Bahati Bukuku alipohojiwa kuhusu taarifa hizo.
Bahati amesema tayari ameripoti kwenye vyombo husika vya uchunguzi ili kumchukulia hatua za kisheria mtu alianzisha uzushi.
Pia Bahati Bukuku amesema kwa sasa yupo studio anatayarisha albam mpya, hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kumpokea na ujio mpya.

0 maoni:

Post a Comment