Friday, December 30, 2016

NIPO TAYARI KUFANYA KAZI NA ALIKIBA MDA WOWOTE REYVAN#johnleo


Hakuna asiyejua kama kuna bifu ambalo sio la pole pole kati ya C.E.O wa WCB WasafiDiamond Platnumz na mtu mzimaAlikiba. Bifu ambalo limekaa kibiashara zaidi na hata ushindani katika game.
Waliwahi kusikika Baraka Da Prince ambaye anaonekana kuwa yupo karibu sana na msaniiAlikiba, na hata Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa damu wa msanii Alikiba na wakadai kuwa wao hawapo tayari kabisa kufanya collabo na wasanii wa WCB kutokana na kudai aina ya muziki ambao wanafanya ni tofauti na muziki wao.
Sasa leo Perfect255 imemkamata mkali kutoka WCB Wasafi hitmaker wa ngoma ya Natafuta Kiki Raymond (@rayvanny) na kupiga nae story imekaa vipi kwa yeye kufanya kazi na msanii ALikiba.
Raymond ametusanua kuwa yeye yuko tayari hata sasa hivi kufanya collabo na Alikibakwasababu ni msanii ambaye hana tatizo naye na hata wakikutana huwa wanasalimiana vizuri na kusifiana kwa kazi nzuri ambazo wanafanya.
“Mimi Alikiba nikikutana nae huwa napiga nae story, namsalimia, tunacheka, ananiambia mdogo wangu unafanya kazi nzuri. Hatujawahi kukaa sana kwa muda mrefu lakini ikitokea siku naweza kufanya nae,kwasababu end of the day wote tunafanya muziki na muziki ni biashara, mashabiki wanapenda kuona combination za watu tofauti tofauti, ikitokea nafanya nae.”
Hayo ni baadhi kati ya mengi ambayoRayvanny amefunguka, play hii video hapa chini ili kumsikiliza mwenyewe akifunguka.

0 maoni:

Post a Comment