Thursday, December 15, 2016

MAJIBU YA SELIKALI KWA WALIMU WANAOSUBILI AJIRA#johnleo

December 15 2016 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alikutana Dodoma na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu ili kujadili namna sahihi ya kuboresha sekta hiyo katika kipindi cha awamu ya tano ambapo katika baadhi ya vitu alivyogusia ni pamoja na suala la ajira kwa walimu.
Waziri Ndalichako amesema…>>>’Utaratibu wa kuajiri tunauboresha, zamani ilikuwa ukisoma ualimu unapangiwa sehemu ya kazi bila hata kuhakikiwa lakini sasa ni lazima kila anayemaliza mafunzo ahakikiwe kwanza ndipo hatua zingine zinafuatwa‘ –Pro. Joyce Ndalichako
Tumebaini kwamba serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwa kuajiri watu wasiokuwa na sifa, tayari katibu mkuu wa wizara yangu ameshatoa tangazo kwa wahitimu wote waliomaliza mafunzo ya sayansi mwaka 2015 wawasilishe vyeti vyao ili vihakikiwe‘ –Pro. Joyce Ndalichako
Na wale watakaoonekana wana vyeti visivyokuwa na mashaka ndio watakaopata nafasi kwahiyo zoezi la ajira kwa walimu limeanza hivyo tunaamini tatizo la ajira kwa walimu haliakwisha lakini tutakuwa tumelipunguza kwa nafasi kubwa‘ –Pro. Joyce Ndalichako
unaweza kuendelea kumsikiliza Pro. Joyce Ndalichako kwenye hii video hapa chini…

0 maoni:

Post a Comment