Thursday, December 15, 2016

BARAKA DA PRINCES AWACHANA WATU WANAOPONDA KUMSAIN KWENYE REBO YAKO#johbleo

Msanii Baraka The Prince ambaye hivi karibuni ametangaza kumsaini Lord Eyes kuwa chini ya lebo yake ya kurekodi ya BANA,amewajibu watu wanao ponda kitendo hicho wakisema ni jambo la aibu, na kuwaambia wana ufinyu wa mawazo.
barakahtheprince_-20160916-0002Baraka The Prince
Akizungumza na EA Radio Baraka amesema kama msanii na mfanyabiashara kupitia muziki, hawezi akadharau sehemu ambayo inaweza ikamuweka vizuri kikazi au kum- fikisha mbali, kwa sababu tu ya kujiona ana muda mrefu kwenye game (legend) au anaweza sana.
“Ngoja nikwambie kitu, huo ni ufinyu wa uchanganuaji na kupambanua kitu, kama hii ni biashara na mtu ambaye anafanya muziki kama biashara, otherwise kama unafanya muziki kwa sifa kwamba mi ni legend, mi ni msanii wa kitambo siwezi kusajiliwa na msanii mpya, hayo ni mapungufu, kama mtu unafanya muziki kama kazi ambayo inaweza kukuingizia kipato maisha yako yakaenda, huwezi ukabagua pa kufanya kazi au panapoweza kuwa na maslahi”, alisema Baraka.
lord eyezLord Eyes
Hata hivyo Baraka amesema yeye kumsaini Lord Eyes haimaanishi kuwa ndiyo anajua sana kuliko wengine, kwani hata hivyo hatahusika moja kwa moja katika kusimamia kazi za wasanii, isipokuwa kuna watu ambao wamewekwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo ambao wana uzoefu mkubwa kuliko yeye.
“Sina maana kwamba mimi ndo naweza sana, kwanza siyo mimi nitakaye kuwa nasimamia, kuna mameneja ambao wako muda mrefu kwenye industry, wanaijua vizuri industry mi nitakuwa mtu ambaye nafuatilia kazi au tuseme kama mkurugenzi wa kampuni, imefika hatua nahitaji kuwa na team pamoja na nguvu yangu”, alisema Baraka The Prince
sindano.blogspot.com

0 maoni:

Post a Comment