Saturday, December 10, 2016

RAISI WA GAMBIA AKATAA MATOKEO YA UCHAGUZI#johnleo

Rais wa Gambia akataa kukubali matokeo ya uchaguzi alioshindwa na upinzaniImage copyrightREUTERS/AFP
Image captionRais wa Gambia akataa kukubali matokeo ya uchaguzi alioshindwa na upinzani
Mtu aliyechaguliwa juma lililopita kuwa rais mpya wa Gambia amesema kuwa rais wa sasa, Yanya Jammeh, amevuruga sifa ya taifa hilo kidemokrasia kwa kukataa kukubali kushindwa katika uchaguzi.
Kundi la kusimamia shughuli za kuandaa kukabidhiana madaraka limesema kuwa rais Mteule, Adama Barrow, na wafanyakazi wake wako salama, baada ya Rais Jammeh, kubadilisha msimamo wake kuwa hakushindwa uchaguzi.
Rais Jammeh alisema kuwa kura zilihesabiwa vibaya na akatoa wito kuwa uchaguzi urudiwe.
Msemaji wa serikali alisema kuwa mkuu wa majeshi nchini anamuunga mkono Bw Barrow.
Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu, Banjul, umetoa wito kwa wanajeshi kuheshimu matakwa ya watu wa Gambia.
Ripoti zinasema kuwa wanajeshi wameweka mifuko ya changarawe katika maeneo mbalimbali jijini kama vizuizi.
Serikali katika taifa jirani la Senegal imetoa wito kwa rais Jammeh kukabidhi madaraka kwa mshindi kwa njia ya amani.
Kukubali kushindwa kwa awali kwa rais Jameh kuliwapa matumaini raia walioona kama mwisho wa utawala wa kimabavu wa zaidi ya miongo miwili ulikuwa umekamilika.

0 maoni:

Post a Comment