Friday, January 20, 2017

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAMTAMBULISHA BENJAMINI SITTA KUWA MEYA HALALI WA KINONDONI#johnleo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtambua Mh. Benjamin Sitta kuwa meya wa Kinondoni. Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili (Ukawa).

Kama mnakumbuka siku ya uchaguzi polisi waliwakamata baadhi ya viongozi na wajumbe wa UKAWA sambamba na ongezeko la wajumbe batili upande wa CCM akiweno Dr. Tulia.

Kesi hii ilifunguliwa dhidi ya Afisa Utawala wa Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Samweli Sita ( aliyetangazwa kuwa Meya) na Manyama Mangaru ( aliyetangazwa kuwa Naibu Meya)

Rejea uzi: CHADEMA imefungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga ushindi Meya wa Kinondoni

0 maoni:

Post a Comment