Friday, January 20, 2017

BEN KINYAIYA AELEZA TUHUMA ZA USHOGA ASEMA WATU WASIMFATILIE MAISHA YAKE#johnleo

img-20161010-wa0014
Wengi wanamfahamu kupitia shoo zake za runinga zilizompa umaarufu mkubwa, zikiwemo Afro Beats alipokuwa East Africa TV, Ben & Mai Live alipokuwa TBC, Mama Land alipokuwa Clouds TV na sasa Kinyaiya’s Corner akiwa Channel Ten, namzungumzia Beny Kinyaiya ambaye leo tunaye kwenye Mtu Kati.
Mwandishi wetu alifanya mahojiano na Kinyaiya ambapo alifunguka mambo mbalimbali, ikiwemo tuhuma zinazomuandama kwa kipindi kirefu, za madai ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga), uhusiano wake wa kimapenzi na wanawake mbalimbali, pamoja na ishu zinazomuweka mjini.
Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Mtu Kati: Mambo vipi Beny.
Kinyaiya: Poa tu!
Mtu Kati: Ukiachilia mbali utangazaji wa runinga, una ishu gani nyingine zinazokuweka mjini?
Kinyaiya: Mimi ni mfanyabiashara, mjasiriamali na msanii. Nina biashara zangu kibao mjini lakini siwezi kuzitaja hadharani, kama hiyo haitoshi, namiliki baa, inaitwa Kinyaiya’s Pub, iko pande za Kinondoni.
Mtu Kati: Hongera kwa mafanikio hayo, vipi kwenye baa yako umewaajiri watu wangapi unaowalipa mshahara?
Kinyaiya: Nimeajiri watu nane, wote mwisho wa mwezi naingia mfukoni na kuwalipa mshahara.img-20161010-wa0022
Akiwa katika pozi.
Mtu Kati: Kwa kipindi kirefu ulikuwa ukifanya kazi kwa karibu na Maimartha Jesse, ni kweli kwamba mlikuwa na uhusiano wa kimapenzi na sasa hamfanyi tena kazi pamoja kwa sababu mmemwagana?
Kinyaiya: Watu wamekuwa wakituhisi vibaya mimi na Mai kwa kipindi kirefu lakini si kweli, Maimartha kwangu ni kama dada na pia kama ndugu. Tumekaa pamoja kwa miaka kibao, tunajuana fresh wala hatujakutana jana au juzi, yaani tangu kitambo. ‘Inshort’ ni mtu wangu wa karibu na tunaheshimiana sana, hayo mengine ni maneno tu ya watu.
Mtu kati: Umri unasonga, vipi umeshaoa au una mpango wa kufanya hivyo hivi karibuni?
Kinyaiya: Bado sijaoa ila nina mtu wangu wa kudumu ambaye Mungu akitujaalia tutafunga ndoa.
Mtu Kati: Vipi katika kupigapiga ‘gemu za nje’, umewahi kupata mtoto au watoto?
Kinyaiya: Yaah! Nina watoto wawili, wa kwanza anaitwa Ben Kinyaiya Junior, ana miaka minne na nusu na wa pili anaitwa Nilla, huyu ni wa kike na ana miaka mitatu.
Mtu Kati: Umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke staa? Ulikumbana na changamoto zipi?
Kinyaiya: (Anasita kidogo), ndiyo nimewahi kutoka na staa lakini ni miaka mingi iliyopita. Unajua mapenzi na staa lazima yana changamoto, zilikuwepo nyingi lakini si unajua tena ndiyo maisha ya kistaa. Ni kama mimi sasa hivi, ukimuuliza mtu wangu ni changamoto gani anakumbana nazo kuwa na mimi, lazima zitakuwa nyingi.
Mtu Kati: Kuna kipindi ulipotea Bongo na kutimkia Uingereza, ikaja kuelezwa kwamba kuna mwanamke mtu mzima alikuwa anakulea, mnaishi kinyumba. Unalizungumziaje hili?
Kinyaiya: Yaah, ni kweli lakini ni siku kibao zilizopita. Nilikuwa na mwanamke nchini Uingereza ambaye nilikutana naye kwenye mishemishe zangu za kibiashara, si unajua mi huwa naenda sana nje kibiashara Hakuwa ananilea isipokuwa alikuwa ni mpenzi wangu, baadaye tukashindwana.
Mtu Kati: Wewe ni miongoni mwa vijana wa kiume wanaopenda sana kujipamba na kutoka ‘bling bling’, ni usumbufu gani unaoupata kutoka kwa akina dada?watoto
Akiwa na watoto wake.
Kinyaiya: Usumbufu ni mkubwa, kama unavyojua tena mimi ni staa halafu najipenda. Na sijaanza kusumbuliwa leo wala jana, tangu nikiwa shule ya msingi, sema huwa najua namna ya kukabiliana nao.
Mtu kati: Kwa muda mrefu kumekuwa na madai ambayo hayajathibitishwa kwamba unajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga), unalizungumziaje hili?
Kinyaiya: Ni mawazo yao tu, kwanza nikwambie mimi huwa siabudu majungu. Watu walianza kunizungumzia vibaya kitambo wakinihusisha na hayo mambo, wengine wakawa wanasema eti hawajawahi kuniona na
mwanamke, nikawapuuzia tu. Baadaye kibao kikageuka, wakaanza kuniita eti mimi ni malaya kwa sababu nina wanawake wengi, pia sikuwajali. Nikaendelea na maisha yangu na sasa hivi ndiyo kama hivyo tena, tayari nina watoto wawili, waliokuwa wakinizushia mambo mabaya wote wamenyamaza kimya.
Mi nafanya shughuli zangu za kimaendeleo, sina haja ya kujibizana na watu wanaozusha maneno ya uongo juu yangu, kama mtu anahisi mimi nina matatizo yoyote basi aniunganishe na dada yake atampa majibu (anacheka).
Mtu Kati: Unawazungumziaje wasanii ambao licha ya ukongwe wao na majina yao makubwa, hawana chochote cha kujivunia kimaisha tofauti na wewe ambaye una miradi kadhaa?
Kinyaiya: Nawaambia wasanii wajitambue, mambo ya kuwa na jina kubwa halafu mfukoni huna kitu yalishapitwa na wakati, muhimu ni kutumia vipaji kuwekeza kwenye vitega uchumi.
Mtu kati: Ahsante kwa ushirikiano wako Beny.
Kinyaiya: Pamoja sana, nina kazi zangu kibao nataka kuzitoa katika ujio wangu mpya, zikiwa tayari tutawasiliana mashabiki zangu wajue, kuna video, kuna filamu na projekti nyingine kibao zinakuja.
Kinyaiya: Ni mawazo yao tu, kwanza nikwambie mimi huwa siabudu majungu. Watu walianza kunizungumzia vibaya kitambo wakinihusisha na hayo mambo, wengine wakawa wanasema eti hawajawahi kuniona na mwanamke, nikawapuuzia tu. Baadaye kibao kikageuka, wakaanza kuniita eti mimi ni malaya kwa sababu nina wanawake wengi, pia sikuwajali. Nikaendelea na maisha yangu na sasa hivi ndiyo kama hivyo tena, tayari nina watoto wawili, waliokuwa wakinizushia mambo mabaya wote wamenyamaza kimya.
Mi nafanya shughuli zangu za kimaendeleo, sina haja ya kujibizana na watu wanaozusha maneno ya uongo juu yangu, kama mtu anahisi mimi nina matatizo yoyote basi aniunganishe na dada yake atampa majibu (anacheka).kujibizana na watu wanaozusha maneno ya uongo juu yangu, kama mtu anahisi mimi nina matatizo yoyote basi aniunganishe na dada yake atampa majibu (anacheka).

0 maoni:

Post a Comment