Wednesday, January 18, 2017

KAULI YA MADEE BAADA YA NAY WA MITEGO KUSEMA WIMBO WAKE NI MBAYA#johnleo


Usiku wa jana rapper Nay wa Mitego alizua gumzo katika mitandao ya kijamii kwa kupost picha katika mtandao wa Instagram na kuweka caption yenye utata ambayo wengi waliichukulia kama dis kwa wimbo mpya waMadee unaoitwa Hela.
PhotoGrid_1484684507012
Post ya Nay wa Mitego
Sasa Perfect255 imepiga story na Madeekuhusiana na post hiyo ya hasimu wake Nay wa Mitego na ana lipi la kuongea juu ya hilo.
” Yale ni maoni yake ambayo kila mtu anao uwezo wa kusema lakwake, mimi sina uhakika sana kama amegusa wimbo wangu, kwasababu hajanitaja ila kitu ambacho nimekiona ni watu wengi ndio ambao wamenitag mimi. Lakini muziki wangu ni muziki wa serikali ya Manzese, kama unavyojua serikali inapofanya kitu wizara zote lazima zijue, yeye hayupo kwenye serikali yangu ndio maana haelewi.” AlisemaMadee.
Pia Madee aliongeza kuwa “Huwezi kui-judge nyimbo kwa siku moja, ukii-judge nyimbo kwa siku moja utakuwa muongo sana. Vitu hivyo tumekwisha viona watu wengi sana wamefeli kwa ku-judge wimbo kwa siku moja halafu baada ya siku kadhaa wanajifungia vyumbani mwao wakiusikiliza huo huo wimbo.”
Play  hii video hapa chini uweze kumsikilizaMadee akifunguka kuhusiana na kauli hiyo yaNay wa Mitego.

0 maoni:

Post a Comment