Monday, February 27, 2017

Wakili Peter Kibatala Amwaga chozi hadharani mbele ya Majaji...Ni kuhusu kinachoendelea Mahakamani juu ya kesi ya Godbless Lema

Wakili Peter Kibatala Amwaga chozi hadharani mbele ya Majaji...Ni kuhusu kinachoendelea Mahakamani juu ya kesi ya Godbless Lema


Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumnyima haki.

Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu (Lema) kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki.

“Tunaomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikai (DPP) muwe makini sana maana mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua Mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushitua sana,” alisema huku akishauriana na wenzake mara kwa mara kwa masikitiko.

Aliendelea kusema kuwa ofisi ya DPP inaitia najisi taaluma hiyo, kitu kipo wazi ila wanafanya vitu vya ajabu na havipendezi.

Alihoji jaji Luanda kuwa “Tumesoma faili lote tunashangaa hivi kweli ofisi ya mwanasheria mkuu ina wanasheria kweli na kama wapo kwa nini huyu mtu (Lema) awe ndani mpaka leo?”.

Alisema kwa kuwa mikono yao kisheria imefungwa hawawezi kufanya chochote kwa leo na kuwataka Mawakili upande wa Lema kurudi Mahakama Kuu, kuendelea na maamuzi ya dhamana.

Hali hiyo ilitokana na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi kusimama mahakamani hapo na kuomba kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa ipo nje ya uwezo wake.

“Waheshimiwa Majaji baada ya timu yetu ya wanasheria kupitia kwa kina rufaa hii kwa sababu zisizozuilika tumeona hatupo tayari kuendelea na rufaa hii, maana hatukupeleka kusudio (Notisi) kwa msajili muda ulipita, hivyo tunaomba kuiondoa na uamuzi wa kuiondoa rufaa hii tumeufikia Ijumaa muda uliisha kuja mahakamani,”.Alisema Nchimbi.

Baada ya kuwasilisha ombi hilo, Wakili wa Lema Peter Kibatala, alisimama na kusema upande wao hawana pingamizi ila waliomba hoja za awali za rufaa hiyo ziondolewe Mahakamani hapo bila kunakiliwa.

Baada ya ombi hilo Jaji Kipenka Mussa alipokea kwa niaba ya Majaji wenzake na kukubali ombi la kuiondoa rufaa hiyo namba 9/2017.

Aidha Jaji Luanda alimkaribisha jaji Stella Mugasha pia kuongea kwa niaba yao ambapo alisema mahakama imekubali ombi la pili la kuiondoa rufaa namba 10/2017, baada ya Wakili Paul Kadushi kuomba kuiondoa pia.

Wakili wa Lema Peter Kibatala, alilazimika kusimama tena Mahakamani hapo kusema kuwa upande wao unasikitika kuona ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP wanatumia Mahakama kwa njia ya kumnyima haki mteja wao, hivyo aliomba mahakama hiyo iwatatulie tatizo la kisheria lililojitokeza hadi mteja wao awe ndani hadi sasa.

Friday, February 24, 2017

Thursday, February 23, 2017

Tatizo LA miguu kuwaka moto mpaka unashindwa kutembea kwa ushauri soma hapa#johnleo


Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.
burning-feet.png

Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.


Ushauri, Kinga na Tiba...



Mrejesho/Ushuhuda

U-HEAD | kitale awaponda ney na madee kupata taarifa zaidi ingia hapa chuni#johnleo


    Moja kati ya story ambazo zilimake headlines kinoma siku ya jana ni pamoja na post ya muigizaji Kitale katika page yake ya Instagram.
    Post ambayo ilichukuliwa kama diss kwa wasanii Nay wa Mitego na Madee kwa kile kilichoandikwa kwenye post ile kudai kwambaMadee na Nay wa Mitego ni wasanii ambao wanaishi kwa Kiki kila wakitaka kutoa ngoma.

    Soudy Brown amemvutia waya Kitale na kutaka kujua alichomaanisha kwenye post yake. Kitale amefunguka kuwa alichokiandika ndio ambacho amemaanisha.
    Pia kuna story zilienea kwamba Mzee wa Upako amemuonya Nay wa Mitego kwa kitendo chake cha kufungua Kanisa, Sasa majibu ya Nay wa Mitego kwa Mzee wa Upako pia ameyatoa kwenye U-Heard ya leo ambayo yote nimeikusanya na kukuwekea hapa chini.
    Bonyeza play kuisikiliza mwanzo hadi mwisho.

    Friday, February 17, 2017

    Nafasi za ualimu Mkoa wa Iringa, Mtwara na songea soma zaidi#johnleo

    NAFASI ZA UALIMU MKOA WA IRINGA,MTWARA NA SONGEA SOMA NA SHARE KWA RAFIKI

    Teaching & Learning Specialists-Iringa

    Education & Teaching

    Details
    Employer Name: RTI International
    Organization Type: NGO
    Role: Experienced
    Position Type: Full Time
    Location: Iringa
                        Iringa Mjini
    Application Deadline: 28-02-2017
    Listed on: 15-02-2017
    Description Application Instructions
    RTI International is accepting applications from qualified staff for the recently awarded USAID/ Tanzania Tusome Pamoja Program (2016-2021) in Tanzania. The 5-year program will assist the Ministry of Education to replicate and scale up reading, writing and arithmetic improvement interventions in schools with an emphasis on curriculum and materials development for Grades 1-4 in Swahili and English. On behalf of the USAID/Tanzania, RTI will work with regional, district, and ward personnel to implement reading, writing, and arithmetic reforms in Five regions of the country, with support given to approximately 3000 public primary schools in the selected regions. Additionally, Tusome Pamoja will implement activities to engage communities and parents to further the goals of improved student learning outcomes.
    We are accepting expression of interests (CV/Resumes) for the following positions


    3. Teaching & Learning Specialists (T&L) to be based in MTWARA, RUVUMA& IRINGA
    The T&L Specialist will support Local Government Authorities (LGA) to improve mastery of early Grade Reading Writing and Arithmetic skills among standard I-IV Students. S/he will work closely with LGA's and implement INSET training, monitoring and coaching in respective Region.

    Qualifications
    : Bachelor Degree in Education with 06-years' experience OR, A Master's Degree in Education with 03- years' experience preferably on a USAID/USG or other donor-funded project in Tanzania. -
    Relevant experience in development, including education reforms, teaching training, coaching & mentoring, literacy and research. Experience and proven ability to develop and maintain relationships with Government counterparts and other Stakeholders. Excellent communication skills in English and Kiswahili languages.
    To apply please email your CV/ Resume and Cover Letter only through APPLYbelow Please indicate name of the position that you are applying for in the Subject Line of your Application. Only short-listed candidates will be contacted. RTI International is proud to be an equal opportunity employer.
    CLICK HERE TO APPLY 

    Nafasi za kazi 100 hospitali ya Ifakala health institute#johnleo


    Nurse Midwife (x46)

    Medical & Dental, Research, Monitoring & Evaluation, Science

    Details
    Employer Name: Ifakara Health Institute (IHI)
    Organization Type: NGO
    Role: Entry Level
    Position Type: Part Time
    Location: Dar Es Salaam
                        Kinondoni, Mikocheni
    Application Deadline: 28-02-2017
    Listed on: 13-02-2017
    Description Application Instructions Mode of Application: All candidates meeting the above job requirements should channel their application letters with detailed curriculum vitae (CVs) showing contact address, e-mail, telephone numbers, and photocopies of academic and professional certificates to the address below. Please indicate position in the subject of the email.
    The Chief Human Resources Officer
    Ifakara Health Institute, 
    Plot 463, Kiko Avenue, 
    PO Box 78,373, 
    Mikocheni, 
    Dar es Salaam

    Medical Attendants (x10)

    Medical & Dental, Research, Monitoring & Evaluation, Science

    Details
    Employer Name: Ifakara Health Institute (IHI)
    Organization Type: NGO
    Role: Experienced
    Position Type: Part Time
    Location: Dar Es Salaam
                        Kinondoni, Mikocheni
    Application Deadline: 28-02-2017
    Listed on: 13-02-2017
    Description Application Instructions Mode of Application: All candidates meeting the above job requirements should channel their application letters with detailed curriculum vitae (CVs) showing contact address, e-mail, telephone numbers, and photocopies of academic and professional certificates to the address below. In the application letter, the applicant should also state why s/he is interested in this position. Please indicate position in the subject of the email.
    Chief Human Resources Officer, 
    Ifakara Health Institute, 
    Kiko Avenue, Mikocheni, 
    P.O.Box 78373,
    Dar es Salaam.
     

    Field Interviewers (x4)

    Medical & Dental, Research, Monitoring & Evaluation, Science

    Details
    Employer Name: Ifakara Health Institute (IHI)
    Organization Type: NGO
    Role: Experienced
    Position Type: Part Time
    Location: Dar Es Salaam
                        Kinondoni, Mikocheni
    Application Deadline: 28-02-2017
    Listed on: 13-02-2017
    Description Application Instructions Mode of Application: All candidates meeting the above job requirements should channel their application letters with detailed curriculum vitae (CVs) showing contact address, e-mail, telephone numbers, and photocopies of academic and professional certificates to the address below. In the application letter, the applicant should also state why s/he is interested in this position. Please indicate position in the subject of the email.
    Chief Human Resources Officer, 
    Ifakara Health Institute, 
    Kiko Avenue, Mikocheni, 
    P.O.Box 78373,
    Dar es Salaam.

    tudy Coordinator

    Medical & Dental, Research, Monitoring & Evaluation, Science

    Details
    Employer Name: Ifakara Health Institute (IHI)
    Organization Type: NGO
    Role: Experienced
    Position Type: Full Time
    Location: Morogoro
                        Kilombero
    Application Deadline: 25-02-2017
    Listed on: 13-02-2017
    Description Application Instructions
    Mode of Application: All candidates meeting the above job requirements should channel their application letters with detailed curriculum vitae (CVs) showing contact address, e-mail, telephone numbers, and photocopies of academic and professional certificates to the address below. In the application letter, the applicant should also state why s/he is interested in this position. Please indicate position in the subject of the email.
    Chief Human Resources Officer, 
    Ifakara Health Institute, 
    Kiko Avenue, Mikocheni, 
    P.O.Box 78373,
    Dar es Salaam.

    tudy Coordinator – SDA project

    Medical & Dental, Research, Monitoring & Evaluation, Science

    Details
    Employer Name: Ifakara Health Institute (IHI)
    Organization Type: NGO
    Role: Experienced
    Position Type: Full Time
    Location: Dar Es Salaam
                        Kinondoni, Mikocheni
    Application Deadline: 20-02-2017
    Listed on: 13-02-2017
    Description Application Instructions
    Mode of Application: All candidates meeting the above job requirements should channel their application letters with detailed curriculum vitae (CVs) showing contact address, e-mail, telephone numbers, and photocopies of academic and professional certificates to the address below. In the application letter, the applicant should also state why s/he is interested in this position. Please indicate position in the subject of the email.
    Chief Human Resources Officer, 
    Ifakara Health Institute, 
    Kiko Avenue, Mikocheni, 
    P.O.Box 78373,
    Dar es Salaam.

    Friday, February 10, 2017

    Spika wa bunge atoa onyo kwa selijali na jeshi la polisi kuwakamata wabunge ovyo msikilize#johnleo

    Spika wa bunge Job Ndugai leo wakati wa Bunge kuahirishwa amesimama na kuzungumzia ishu ya baadhi ya Polisi wa Tanzania kushika Wabunge bila yeye kupewa taarifa ambapo amesisitiza ‘hatuwezi kwenda namna hiyo’
    Amesema hadhi ya Bunge iko palepale na kwamba Muhimili wa Bunge hauna ugomvi wowote na serikali, mambo ya Ofisa mmojawapo kusahau mipaka na kuvuka ni lazima yeye aambiwe, unaweza kutazama kila alichosema kwenye hii video

    VIDEO: “Unapotangaza mtu aje Polisi saa 5, wewe ni nani? – MBOWE

    SMS ambayo itamfanya mwanamke akutamani na kukubali haraka#johnlep

    SMS Ambayo Itamfanya Mwanamke Akutamani na kukubali haraka



    Unaweza dhania kuwa kutuma ujumbe mfupi kwa mwanamke ili umsisimue haifai. Lakini kusema kwa hakika, inawezekana kumtumia mwanamke SMS ambayo inaweza kumsisimua na pia kupata atenshen kutoka kwake. Hii inaweza kufanya kazi vizuri iwapo umeingiwa na kibaridi cha kuongea na mwanamke moja kwa moja.

    Kabla ujumbe ufupi kuvumbuliwa, wanaume walikuwa wakifuata mbinu nyingine kuonyesha kuwa wamevutiwa na wanawake waliowapenda. Walikuwa wakituma barua, kuambia rafiki wa rafiki zao ama kuwafuata na kuwapigia mbinja majumbani mwao. Lakini kwa bahati nzuri, hivi sasa kuna SMS, ambazo zina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi hapo kwa hapo kwa mwanamke ili kurahisisha kazi yako ya kutongoza.

    Kabla hujaanza kumvutia mwanamke, ni lazima kwanza umfanye akutambue kwa njia chanya kwanza. Mwanzo haupaswi kutumia SMS kumsisimua mwanamke mpaka ile siku ambayo utapata kumsoma na kumjua zaidi. Lazima ujipatie muda ili ujenge connection kati ya nyinyi wawili ili iweze kufanya kazi. Kufanya hivi kutatoa picha ambayo itajijenga katika akili yake wakati munatumiana jumbe za kimapenzi. Kama ulimpendeza sana ile mara ya kwanza alipokupatia namba yake ya simu, basi itakuwa rahisi kwa mpangilio wako uende sambamba kama vile unavyotarajia.

    Pindi utakapoingia katika level nyingine ya kuliwazika na huyu mwanamke ambaye unamrushia mistari, mwonyeshe vile ambavyo umependezwa na yeye kwa kumsifu. Hakikisha kuwa unakuwa mpole katika SMS zako pia. Kama yuko darasani au kazini, usimtumie jumbe mpaka ule wakati ambao yuko huru na makini wa kujibu texts zako.

    Kama hujui ni wakati gani atakuwa yuko free, unaweza kujaribu kumtext wakati uo huo ambapo amekupatia namba yake ya simu (hakikisha una makinika kama utaamua kumtumia jumbe wakati uo huo ili usionekane kuwa una uhitaji mwingi). Vizuri zaidi wakati unapomtumia huo ujumbe unapaswa umsifie kwa jambo ambalo umeliona wakati ambapo ulikuwa naye awali. Mfano unaweza kumsifia kitu ambacho ulikiona kama vile nguo nzuri, tabasamu lake, macho, mawazo yake nk. Jaribu kuhepa kugusia umbo lake wakati huo.

    Kama umekuwa mkitumiana jumbe kwa muda sasa na mumetoka deti mara moja au mbili, unaweza kuanza kuingiza na kugusia maswala ya mapenzi katika SMS zenu ili kuanza kupasha misuli kwa mambo ambayo unamwandalia usoni.
    Kutokana na mistari ambayo umekuwa ukiisoma kwa mitandao ama kuiskia kwa marafiki zako, unaweza kuanza kumtext mwanamke huyu mara moja moja huku ukitulia ukiskilizia kama atakujibu kwa kukubaliana nawe ama kukupinga. Ukiona kama kila ujumbe anaoujibu anajibu kwa njia chanya, basi ni wakati wa kwako usichelewe tena bali uhakikishe ya kuwa unatumia mbinu ambayo utaingiza mawazo yako kwa akili yake na hatokusahau milele – huwezi jua, labda meseji utakayomtumia baadaye itakuwa ndio meseji ya kumfanya ajeuke kuwa mpenzi wako.

    Thursday, February 9, 2017

    Mwanashelia wa chadema na mbunge wa singida mashariki aachiwa kwa zamana#johnleo

    Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida MAshariki amefikishwa Mahakamani.

    =====

    tundu.jpg
    DAR: Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kutoa lugha ya kichochezi

    ---- Update: 1
    Serikali imeleta hati ya kiapo ambayo inazuia Mh. Tundu Lissu asipewe dhamana.

    Kibatala ambaye ni Wakili wa mtuhumiwa amepinga kuwa hicho kiapo kilicholetwa hakina mantiki yoyote kisheria kwa sababu kimeletwa kwa kuvizivizia. Halafu kina makosa mengi, kinazungumzia kuhusu kesi nyingine ambazo amewahi kutuhumiwa nazo, ambazo hazina uhusuiano na kesi ya leo. Kiapo hakitaji kimewahi kutolewa mbele ya Mwanasheria gani, kimepigwa muhuri tu.

    Kibatala amelalamika kwamba uwepo wa kesi zingine hata kama zingekuwa mia moja (100) bado haziwezi kuzuia mtuhumiwa kupewa dhamana.

    Kiapo kilichotolewa na serikali hakionyeshi ni katika Sheria ipi ambazo zinahusiana na hii kesi ili huyu mtuhumiwa asipewe dhamana.

    Wamezungumzia kwamba mtuhumiwa asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake lakini wakashindwa kueleza tangu mwezi wa Januari 2017 alipofanya kosa analotuhumiwa, muda ambao sasa mwezi mzima alikuwa anaishije na labda kama amewahi kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi au kwenye vyombo vyovyote vya dola kuwa anatishiwa usalama wake izingatiwe pia Lissu ni Mbunge. Hawajaeleza popote kwamba usalama wa Lissu unatishiwa kwa namna gani mathalani amewahi kukosowa na risasi wapi na wapi.

    Wakili Kisenyi (tumefanikiwa kupatikana jina moja kwa sasa) ambaye ni mmoja wa jopo la Mawakili wa Serikali linaloundwa na Mawakili wane (4), ameomba dakika 20 ili akapitie vitabu vya Sheria kuangalia makosa yaliyotajwa kuwemo kwenye kiapo chake.

    Hakimu amekataa na kuwaeleza Mawakili wa Serikali kuwa ndiyo maana mlikuja wanne na kuongeza kuwa pamoja na kwamba mliwapatia wenzenu kiapo hapa hapa lakini wao wamejibu kwa hoja nyingi.

    Hakimu ameonekana kutokuwa mnyonge na kutoa dakika 10 tu.

    Kesi itaendelea baada ya muda huo ili hakimu atolee maamuzi na ifahamike kama Lissu atapewa dhamana au lah!

    -----Update: 2

    Wakili wa Serikali, ndugu Kisenyi amekuja kujibu hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi kuhusu hati ya kiapo.

    Wakili Kisenyi anasema Mahakama isiangalie makosa yaliyopo katika hati ya kiapo iliyowasilishwa na Mawakili wa Serikali.

    Anasema mahakama ijiridhishe na mhuri uliopo kwenye kiapo na isihangaike kuangalia kiliapwa kwenye ofisi gani maana mhuri unaonyesha umegongwa na Wakili aliyopo Dar es Salaam.

    Na kuhusu hoja kwamba hakuna facts zinazonyesha kuwa Askari anayemtuhumu Mh. Lissu amepata wapi habari za mtuhumiwa, Wakili Kisenyi amejibu kwamba Askari amezipata kwa njia za Kiintelijensia kwa kuwa yeye Mpelelezi.

    Juu ya hoja ya usalama wa mtuhumiwa, Mawakili wa Serikali wamesema kuwa si lazima uwe usalama mtuhumiwa mwenyewe maana maneno anayoweza kutoa akiwa nje ya mahakama au Polisi yanaweza kusababisha uvunjivu wa Amani kwenye jumuiya nzima na jamii nzima ikahathirika hata kama si yeye pekee.

    Kwa hiyo wameweka msisitizo kuwa kiapo kipo sawa.

    Baada ya kuwasilisha majibu ya hoja, Mawakili wa Serikali wameiomba Mahakama ikubaliane na hati ya kiapo na hivyo imnyime Mh. Lissu dhamana.

    Kesi imeharishwa tena kwa nusu saa. Hakimu atarejea baada ya muda huo kuja kutoa huku

    -----Update: 3

    Dhamana ya Mh. Tundu Lissu ipo wazi!

    Maamuzi juu ya hukumu kama yalivyotolewa na Hakimu.
    • Vifungu vyote vilivyotumiwa na Mawakili wa Serikali kuzuia dhamana havikukidhi mahitaji ya kisheria na hivyo si miongoni mwa sababu zinazoweza kuzuia dhamana
    • Kuhusu masuala ya usalama wa mtuhumiwa, Hakimu kasema hakuna taarifa zozote za kina zilizotajwa kwenye kiapo kuthibitisha kuwa mtuhumiwa au jamii inaweza kuhatarika
    • Kiapo kilichowasilishwa na upande wa Serikali kimekuwa na mapungufu mengi, kimekosesewakosewa kimaandishi na hakikuwa na namba ya kesi wala hakikuonyesha kimechukiliwa wapi
    • Kufuatia maelezo hayo, Hakimu amehitimisha kwa kusema Mh. Tundu Lissu anaruhusiwa kudhaminiwa.
    • Patrick J. Assenga amejitokeza kumdhamini kwa dhamana ya TZS 20,000,000/= (milioni ishirini).
    • Kesi itaendelea tena tarehe 06/03/2017
    • Hali nje ya mahakama ilikuwa ya ulinzi mkali. Askari wenye silaha walikuwa wametanda. Haikuweza kufahamika haraka walikuwa na lengo gani. Lakini dalili zilionyesha walitaka Mh. Lissu aingie mikononi mwao akitoka nje ya mahakama. Vijana wa CHADEMA wameweza kuwachezashere askari na kutoweka na Mh. Lissu kuelekea kusiko julikana.
    Tunaendelea kukuhabarisha kadri matukio yatakavyotokea.


    L1.jpeg
    L2.jpeg
    ------
    Rejea:

    Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa bungeni Dodoma

    Tundu Lissu ahojiwa Kituo cha kati kwa kutoa maneno ya Kichochezi ya Uwepo wa njaa nchini