Thursday, August 23, 2018
Tuesday, August 21, 2018
Siwezi kuambatana na dogo janja kila mtu na kazi yake Irene Uwoya #johnleo
Mwigizaji Irene Uwoya ambae ni Mke wa Msanii wa Bongofleva Dogo Janja amesema hawezi kuambatana na Mume wake huyo kwenye kila tukio kama ambavyo Mashabiki wengi wanavyotaka.
Irene amesema “Jamani ni kazi…. si kila mtu ana kazi zake? sasa tukiongozana hivyo nitafanya kazi zangu saa ngapi? hapana aisee muda huu ni wa kuambatana au kufanya kazi?”
Friday, December 15, 2017
Raid Magufuli: wanaosema vyuma vimekaza waweke gilisi#johnleo
Rais John Magufuli amesema vyuma vikikaza vinatakiwa kuwekwa grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa.
Amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).
Rais Magufuli amesema waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali ndiyo wanaosema vyuma vimekaza.
“Vyuma vimekaza na bado vitavunjika kabisa nawashauri muweke grisi,” amesema.
Msemo wa vyuma vimekaza umekuwa maarufu katika siku za karibuni ukiwa na maana maisha yamekuwa magumu.
Rais Magufuli amesema alipoingia madarakani alikuta changamoto nyingi zikiwemo za wafanyakazi hewa, vyeti feki na ufisadi.
Amesema baada ya kudhibiti, watumishi wa umma 12,000 wamepatikana na vyeti feki wakiwemo walimu 3,655 tangu walipoanza kuhakiki.
Amesema uhakiki huo ulibaini watumishi hewa 20,000 na kwamba, Serikali ilikuwa inapoteza fedha nyingi kuwalipa mishahara.
“Kila kitu kilikuwa hewa hata mapenzi inawezekana yalikuwa hewa,” amesema Rais Magufuli.
Amesema kutokana na udhibiti wa fedha za Serikali ni lazima watu waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali watalalamika kuwa vyuma vimekaza.
Kuhusu madai ya walimu, amesema Sh25 bilioni wanazoidai Serikali zitalipwa baada ya uhakiki kumalizika
==>Msikilize hapo chini==>>
Majina ya wanajeshi waliopoteza uhai huko congo,#johnleo
Haya ni majina ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani.
Wanajeshi hayo ni;
1. Hamad Haji Bakari,
2. Chazil Khatibu Nandonde,
3. Idd Abdallah Ally,
4. Juma Mossi Ally,
5. Ally Haji Ussi,
6. Pascal Singo,
7. Samwel Chenga,
8. Deogratius Kamili,
9. Mwichumu Vuai Mohamed,
10. Hassan Makame,
11. Issa Mussa Juma,
12. Hamad Mzee Kamna,
13. Salehe Mahembano na
14. Nazoro Haji Bakari.
Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.
Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.
Wednesday, December 13, 2017
Maelezo mafupi kuhusu blog ya johnleo inayomilikiwa na johnleo#johnleo
Naitwa john Marco ni kijana mjasiliamali nimezaliwa Tanzania mkoa wa simiyu katika wilaya ya bariadi kijiji cha old maswa kila mtu amezaliwa na kipaji chake na pia ana ndoto yake nina kipaji na pia Nina ndoto, kwa sasa tayari nina blog yangu ambayo huwa nafanya post za aina mbalimbali natamani siku moja nije kuwa na blog kubwa kama ya millardayo au michuzi blog na kadri mda unavoenda nitakuwa nabadilisha mwonekano was blog yangu jina la blog inaitwa johnleo.blogsport.com ukiitaji zaidi unanitafuta kupitia Facebook ambapo unaweza kuzipata moja kwa moja pia unaweza kunitafuta kupitia www.sindano.com ninachohitaji kwenu ni sapoti yenu mwezi ujao nitakuwa na account ya YouTube ambayo nitakuwa naweka huko pia kwa jina hilohilo la johnleo. By johnleo
Rais Magufuli: Amuagiza Waziri wa Fedha kuhakikisha malipo kwa kutumia fedha za kigeni yanadhibitiwa.johnleo
Habari zenu wakuu
Benki ya CRDB inafungua tawi lake jipya mjini Dodoma katika Jengo la LAPF.
Tukio hili liko live TBC1.
Pamoja na wageni wengne yupo Mh. John Pombe Magufuli ambaye ni mgeni rasmi, katibu mkuu wizara ya fedha, mawaziri, spika wa bunge, mkurugenzi wa CRDB DR. Charles kimei na wageni wengne mbalimbali.
Kwa mujibu wa mh. Rais yeye ni miongoni mwa wateja wa CRDB na anaamini CRDB ina mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda na kutoa ajira kwa watanzania.
=======
Rais Magufuli: Amuagiza Waziri wa Fedha kuhakikisha malipo kwa kutumia fedha za kigeni yanadhibitiwa.
> Asema alizuia Mkataba ulioandaliwa na Benki Kuu uliopanga kulipa kwa Dola za Kimarekani. Asisitiza suala hili likiendelea Wasimlaumu.
Rais Magufuli: Pale Benki Kuu(BOT) kuna watu 17 wenye PhD lakini waliruhusu Benki moja kufanya biashara hapa nchini bila kutambua kuwa ni ya kibababishaji.
> Ilipozuiwa Marekani na wao ndio wakashtuka.
Rais Magufuli: Mabeki ambayo hayafanyi vizuri BoT isisite kuyafungia na kuacha mambo ya kubebana bebana
> Ni bora kubaki na beki 5 zinazofanya vizuri kuliko kuwa na benki nyingi zisizo na tija
Rais Magufuli: Najua Makao Makuu yenu yapo Dar lakini nitoa wito kwenu CRDB muangalie utaratibu wa kujenga Makao Makuu hapa Dodoma
> Kwanza itasaidia kutangaza benki yenu na hata mkiwa na jambo mtasaidiwa haraka kwa sababu hata Makao Makuu ya Serikali yatakuwa hapa

Saturday, December 9, 2017
Baada ya JPJ Magufuli kuwasamehe babu Seya na familia yake wasanii waguswa na kuandika haya#johnleo
Siku ya December 9, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa Familia ya Babu Seya, msamaha huo ameutoa wakati wa Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara Mjini Dodoma wakati akihutubia.
Baada ya msamaha huo wa Rais baadhi ya mastaa wameonesha kuguswa na msamaha huo ambapo wameamua kuandika kupitia kurasa zao za Instagram…na baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Mchekeshaji Katarina Karatu, Dkt. Cheni, Mh Temba, na Petit Man Wakuache, Afande Sele…
“Mungu ni mwema #salutejpm“ – Mh. Temba
“Hao uraian Asanteee Rais wangu Mzalendo wewe ndiye Jembe letu mh John Pombe Magufuli Barikiwa sana” – Dkt. Cheni
“Uhuru day pino babaaaaa JPM Tishaaaaa mzee baba” – Petitman Wakuachetz
“Saba mara sabini….Kongole mr president Jpm” – Afande Sele
BREAKING: JPM ameagiza kuachiwa huru kwa Babu Seya na Familia yake
Hatimae Rais John Pombe Magufuli leo aiachia huru familia ya babu Sega kuanzia leo wapo huru#johnleo
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza
Yametimia katika sherehe za Uhuru 2017. Katiba ya JMT Ibara ya 45 yatumika.
Karibuni kwa maoni na povu.
Rais John Magufuli akiwa kwenye kilele cha miaka 56 ya Uhuru amesemehe wafungwa waliohukumiwa kwa vifungo mbalimbali na kunyongwa.
Miongoni mwa waliosamehewa ni wanamuziki Nguza Viking Alias maarufu Kama Babu Seya na Johnson Nguza(Papii Kocha) ambao walihukumiwa kifungo Cha maisha gerezeni kwa kosa la kubaka na kulawiti watoto 10 mwaka 2003 na kuhukumiwa Juni 25, 2004.
Pia Rais Magufuli amemsamehe mzee Matonya mwenye miaka 85 ambae alihukumiwa kunyongwa na ameshakaa miaka 37 baada ya hukumu na miaka Saba mahabusu.
Friday, December 8, 2017
MWANZO MWISHO: Birthday party ya Jackline Wolper 2017 (+video)#johnleo
Ni jibu gani alilotoa pale alipoulizwa ametimiza umri gani? vipi Harmonize na Mpenzi wake walitokea kwenye party baada ya Wolper kuwaalika? tazama hii video hapa chini ujionee
VIDEO | Diamond Platnumz Ft. Rick Ross - Waka waka | Watch/Download#johnleo
VIDEO | Diamond Platnumz Ft. Rick Ross - Waka waka | Watch/Download
Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira atangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Johnleo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira atangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema ameridhika na mwenendo mpya wa Chama hicho chini ya Mwenyekiti wake, Dkt. John Pombe Magufuli na aimeiona CCM inayobadilika, na kuona juhudi za kila mtu, ameiona CCM inayoanza kukataa rushwa, na itaipeleka taifa mbele.
Amejiunga leo kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanyika mjini Dodoma.

Saturday, November 25, 2017
Dr. Lous Shika amefunguka na kusema kwamba amefurahi sana baada ya kusikia kwamba Nyumba za Lugumi ambazoz jana zilifanyiwa mnada wa Marudio zimekosa mnunuzi.#johnleo
Dr. Lous Shika amefunguka na kusema kwamba amefurahi sana baada ya kusikia kwamba Nyumba za Lugumi ambazoz jana zilifanyiwa mnada wa Marudio zimekosa mnunuzi.
Dr. Shika ambae alikuwa mshindi wa kuzinunua nyumba hizo kwenye mnada wa awali lakini alishindwa kukamilisha mashrti ya mnada ya kulipa asilimia 25 ya fedha za manunuzi na kusababisha mnada huo kurudiwa tena jana amesema, kukosekana kwa mnunuzi kwenye mnada huo wa marudio imempa nguvu na kusema kwamba ndani ya wiki mbili atafanya mpango wa kuzilipia nyumba hizo.
"baada ya kusikia kwamba nyumba ambazo nimekuwa nikizihitaji kwa muda mrefu kwamba hazijanunuliwa hata mnada wa leo(jana),hiyo mimi imenipa nguvu,nimefurahi"
"Changu ni changu,basi katika wiki mbili hizi zinazofuata hela itakuwa imeshaingia.Kumbe Mungu amenizunguka bado, yupo pamoja na mimi" .Alisema Dr.Shika
Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia#johnleo
Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia
Rais John Magufuli amesema hakubomoa jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopo Ubungo alipokuwa waziri wa ujenzi kwa kuwa aliogopa kufukuzwa kazi.
Rais Magufuli amesema hayo leo Jumamosi Novemba 25,2017 alipozindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila.
Akizungumza mbele ya waziri mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mizengo Pinda aliyehudhuria uzinduzi huo, Magufuli amesema wakati huo aliogopa baada ya kuzuiwa na waziri mkuu huyo, lakini sasa yeye ndiye Rais hakuna wa kumzuia.
Akizungumzia ubomoaji unaoendelea sasa amesema, “Nilishatoa maagizo, najua Mizengo Pinda kwenye hili alinipinga wakati ule, lakini najua leo hawezi akanipinga kwa sababu mimi ndiye Rais. Wakati ule nilikuwa waziri wake, ndiyo maana nilinyamaza nilijua ninaweza nikafukuzwa, hutakiwi kumpinga mkubwa.”
“Hilo jengo la Tanesco, narudia kama itakuwa ni kubomoa nusu, no problem (hakuna tatizo); kama ni lote hakuna tatizo, pamoja na jengo la wizara ya maji. Najua katibu mkuu wa wizara ya maji yupo hapa ananiangalia, wakaanze kulitoa eneo lililopo kwenye hifadhi ya barabara,” amesema.
Machi 6, 2011 akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato, mkoani Kagera, Pinda ambaye alisifia utendaji wa Dk Magufuli alimwagiza kusimamisha ubomoaji maeneo kadhaa yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara likiwemo jengo la Tanesco hadi Serikali itakapotoa kauli nyingine kuhusu hilo.
Pinda alikuwa akizungumzia hatua ya Dk Magufuli aliyekuwa amewaagiza wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo na wasitarajie kulipwa fidia.
Pinda wakati huo akiwa waziri mkuu alisema spidi (kasi) ya Magufuli ilikuwa kubwa hivyo alimuagiza kusimamisha ubomoaji huo hadi suala hilo litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri.
Pinda, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia 2008 baada ya kujiuzulu kwa Edward Lowassa alisimamisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga upya.
Alisema Serikali inamuamini Magufuli kuwa kiongozi mwenye uwezo na ndio maana ilimpa nafasi akawabane makandarasi wazembe.
Dk Magufuli akiwasilisha bajeti bungeni mwaka 2012/13, alizungumzia ubomoaji akisema siasa iachwe akisisitiza sheria zimepitishwa ikiwamo Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na ya hifadhi ya barabara iliyoanza tangu mwaka 1932.
Alizungumzia jengo la Tanesco alisema liko kwenye hifadhi ya barabara na kwamba hata kama asipolibomoa yeye kuna siku litabomolewa vinginevyo sheria ibadilishwe.
Novemba 15 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Magufuli alimuagiza wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo la Tanesco na Wizara ya Maji, sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.
Chanzo: Mwananchi

Subscribe to:
Posts (Atom)