Sunday, March 26, 2017

Raisi magufuli amemtumbua katibu Mkuu Wa nishati na madini#johnleo

Rais amtumbua Katibu Mkuu Nishati na Madini

SUNDAY , 26TH MAR , 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa kuanzia leo Jumapili machi 26,2017
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ikulu nafasi ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo itajazwa baadae.

Friday, March 24, 2017

HABARI | waziri ashutumu kwa nini nape alionyeshwa bastora kumzuia asiongee na wanahabari# johnleo

Tanzania: Waziri ashutumu askari kwa kuchomoa bastola wakimdhibiti Nnauye

  • 24 Machi 2017
Bw Nchemba akiwa na Rais MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
ImagWaziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari mmoja kuchomoa bastola na kufyatua risasi wakati maafisa wa usalama walipokuwa wanajaribu kumzuia aliyekuwa waziri wa habari kuhutubia wanahabari.
Bw Nchemba, kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kitendo hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika kuadhibiwa.
Amesema amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumsaka mhusika.
"Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana rekodi ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea bastola, sio cha kiasikari, sio cha Kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini," ameandika.
"Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.

Thursday, March 23, 2017

NEWS • walichokiandika baazi ya wanasiasa na mastaa wa bongo baada ya nape kuenguliwa uwazili#johnleo

WALICHO KIANDIKA BAADHI YA VIONGOZI NA MASTAA BAADA YA NAPE KUONDOLEWA KWENYE UWAZIRI WA HABARI, SANAA NA MICHEZO

Alhamis hii jua limechomoza likiambatana na mshtuko mkubwa kwa wananchi wengi wa Tanzania.
Mshtuko huo umetokana na taarifa ya mheshimiwa Nape Nnauye kupokonywa nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii imekuwa habari yenye mpasuko mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nape ameonekana kuwa mtetezi muhimu wa vyombo vya habari kufuatia kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha nzito.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokea ripoti toka kwenye kamati aliyokuwa ameiteua kufanya uchunguzi wa tukio hilo, Nape ameondolewa na kuacha sintofahamu kubwa kwenye mkasa huo.
Mastaa, viongozi na wananchi wametoa maoni yao ambao mengi yanafanana – hawajependezwa na kilichotokea huku wengi wakimwelezea Nape kama shujaaa.
Haya ni baadhi yao:
Zitto Kabwe
Nimezungumza na mbunge wa Mchinga @Nnauye_Nape na kuthibitisha kuwa Ni Kweli ameondolewa kwenye Uwaziri. Nape ni Shujaa wa kizazi chetu
Irene Kiwia
The key resource of ordinary citizens is numbers. And justice will reign on earth and truly will the voice of the people be the voice of God. When there is true awakening of the people, in numbers, it forms the real and conscious public opinion.
B12
Nitakua naota eti……. Ngoja nilale tena then niamke! Maana hii si mara ya kwanza kukutana na ndoto mbaya ya kutisha!!
Nchakalih
Kaka @Nnauye_Nape nakushukuru kwa kunipa mfano wa kutumia kumfundishia mwanangu zion somo la uzalendo! HISTORY will JUDGE you RIGHT!! ðŸ‘ŠðŸ‘Š
Halima Mdee
Naamini ni UZUSHI!!
Edo Kumwembe
Sidhani kama Nape anajali…alilitafuta hili kwa nguvu zote…sidhani kama anajali

Bonge la Nyau
Huyu ni shujaa wangu……
Wema Sepetu
We will Surely Miss U as Our Minister… Tulishakuzoea. Such a way to start Your Morning.. Lets wait for what’s NEXT…. This Is Tooo Much Jamani. This Country Be Full of Surprises Nowadays…. Smh.. Never Knew Nchi ina MaRais wawili… Now I know…. Smh…
Idris Sultan
Raisi akashika Jiwe na Almasi akavipimaaaaaaaa aksema embu katupeni almasi ina’ngaa kijinga jinga tu nimeiambia ing’ae kwani.
Madee‏ 
Sad newz😭😭
Masoud Kipanya
Haya ni mawazo yangu… Ningekuwa @Nnauye_Nape ningekaa KIMYA kabisa
Diva
Nimepata mshtuko wa mwaka ðŸ¤¥. Kama Kijana Mpenda Haki na Mpenda Maendeleo na Ninaejitegemea Nimepata Mshtuko wa Mwaka , Nimejiuliza maswal Kwa uchungu Chozi limetoka ðŸ¤¥ðŸ¤§
Peter Msigwa
Kwa Magufuli bashite ni mhimu na ni bora kuliko Nape ndani ya chama na serikali! Hongera JPM!
Mwana FA
(Alitweet muda mfupi kabla ya habari za kuondolewa uwaziri (Toka mwanzo kabisa wa haya maswahibu,kaka yangu @Nnauye_Nape anaonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa..kisiasa na kibinadamu. Anajua umuhimu wa kufanya ‘vita’ dhidi ya mambo yasiyo sahihi kwa jamii bila dhulma na ukiukwaji wa sheria,na hayumbi kwy kusimamia ukweli.
NA HARINGI ðŸ˜€..SALUTE kaka @Nnauye_Nape …najivunia kusema nakujua,ubarikiwe ndugu yangu)
Baada ya habari hiyo kufahamika alitweet: Aisee..
Aika
Its not dictactorship its being a coward #JustSaying running frm people challenging u ðŸ‡¹ðŸ‡¿

Wednesday, March 22, 2017

HABARI | Huu ndio uamzi wa vyombo vya habari baada ya makonda kuingilia Uhuru wa habari

HUU NDO UAMUZI WA VYOMBO VYA HABARI JUU YA PAUL MAKONDA "MAKONDA NI ADUI WA UHURU WA HABARI HIVYO HAKUNA KUANDIKA WALA KUTANGAZA HABARI ZAKE KUANZIA LEO"

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) limeamua kwa kauli moja kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
“Kuanza sasa, mikutano yake, shughuli zote anazozifanya Dar es Salaam hatutakwenda wala kuripoti chochote,” amesema Katibu wa jukwaa hilo, Neville Meena kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Amesema kama kutakuwa na shughuli ambayo inahusisha kiongozi mwingine pamoja na Makonda, vyombo vya habari vitaripoti bila kumhusisha kwa vyovyote mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam.
“Makonda tutampa total black out ni kazi rahisi tu,” amesema.
“Hatutarajii kuona sura yake kwenye televisheni, hatutarajii kuona sura yake kwenye gazeti wala kusikia sauti yake kwenye redio,” amesisitiza.
Kwenye taarifa yake, TEF imelaani vikali kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media Group usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha.
“Tunaalani vitendo vya Makonda na atakayekiuka na kufanya kazi na Makonda, kitakachomkuta hatutamsaidia. Waandishi,wahariri wote tunakubaliana, sote tunasema halikubaliki na tunalaani vikali vitendo vya Makonda, utekelezaji agizo la kutokufanya kazi na RC Dar unaanza mara moja kwa vyombo vyote vya habari nchini, uamuzi huu unaungwa mkono na UTPC.”
“Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni adui wa Uhuru wa Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru wa habari nchini,” imesema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.
Na Emmy Mwaipopo

HABARI | Barnaba afunguka tuhuma za kuachana na mpenzi wake#johnleo

BARNABA AFUNGUKA KUHUSU KUACHANA NA MAMA STEVE

Moja kati ya story ambazo zilikuwa zinakiki kinoma noma wiki chache zilizopita ni pamoja na kuhusu mahusiano ya Mkali wa Bongo Fleva Barnaba Boy na aliyekuwa mpenzi wake Mama Steve.
Ni mengi yaliongelewa kuhusiana na issue hiyo lakini hatukubahatika kupata nafasi ya kuisikia sauti thabiti kutoka kwa Barnaba akizungumzia kuhusiana na issue hiyo.
Leo kwenye XXL ya Clouds FM Barnaba alikuwa na excluisve interview wakati akizindua ngoma yake mpya inayokwenye kwa jina la Lonely.
Na moja kati ya maswali ambayo Barnaba ameulizwa ni pamoja na hilo kuhusiana na mzazi mwenzake, na mkali huyo amemaliza utata wote kwa kusema kwamba ni kweli yeye na Mama watoto wake (Mama Steve) wametofautiana kwa kipindi kirefu sasa.
“Siwezi kusema kwamba tumeachana wala tumetengana, mimi na Mama Steve tumetofautiana, na ni kwa kipindi kirefu sasa.” Alisema Barnaba.

HABARI | Tanzania ni moja ya nchi ambayo wananchi wake hawana fulaha#johnleo


Tanzania, Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha Duniani.
Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.

Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani yake Denmark, ambayo ilichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayo na ni kwanini.
Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya kati ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. 
Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, huku nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia.

Source: BBC

Sunday, March 12, 2017

MPYA | sawa ya ukimwi yangundulika upya nchini India kwa maelezo zaidi ingia hapa#johnleo

Screenshot_2017-03-11-19-45-31-1.png

MAMILIONI ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) ulimwenguni, sasa wanaweza kupata tumaini jipya baada ya wanasaynsi wa nchini Isreali kugundua dawa ambayo inasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu Ukimwi.

Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Hebrew kilichopo Jerusalem nchini Israeli wamegundua dawa yenye protini ambayo wanadai inaweza kupunguza virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa mgonjwa kwa asilimia 97 ndani ya siku saba tu, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Times la Israel.

Ugunduzi huu mpya sasa unatoa tumaini jipya katika utafutaji wa dawa ya ungonjwa huu ambao mpaka sasa hauna tiba ukiwa umeshaua watu zaidi ya milioni moja kwa mwaka 2015 pekee.

Virusi vya Ukimwi hushambulia chembe chembe nyeupe za damu zinazojulikana kama CD4 ambazo husaidia kupigana na magonjwa yanayoingia mwilini.

Virusi vya Ukimwi huingia ndani ya chembe chembe hai nyeupe na kujizalisha kwa wingi jambo ambalo husababisha uharibifu wa CD4.

CD4 zinapokuwa chini ya 200 kwa kyubiki milimita za ujazo wa damu, mgonjwa anahesabika kuwa tayari ameanza kuugua Ukimwi.

Ugunduzi huo mpya umehusisha majarabio ya dawa hiyo mpya ambayo iliwekwa kwenye damu ya wagonjwa 10 wa Ukimwi iliyokuwa kwenye chupa maalumu kwa ajili ya majaribio.

Sehemu kubwa ya dawa hiyo ambayo ilipewa jina la Gammora na watafiti, ilisababisha uzalishaji wa DNA ya virusi hao ndani ya CD4 iliyoathirika kujizalisha kwa wingi badala ya utaratibu wa kawaida ambao huzalisha moja au mbili.

Hii inasababisha chembe chembe nyeupe zilizojeruhiwa kujiharibu zenyewe na kuzifanya zishindwe kusambaza virusi zaidi.

Majarabia yanahusisha dawa hii mpya ya Gammora yataendelea kukiwa na matumaini makubwa kuwa itaweza kuua asilimia 100 ya seli zilizoathiriwa na Virusi vya Ukimwi.

Abraham Loyter mmoja ya wagunduzi wa dawa hiyo mpya, aliliambia gazeti moja la Israeli kuwa ugunduzi huo mpya unaleta tumaini jipya.

“Tunachokifanya sisi ni kuharibu seli ambazo zimeathirika na kwa hiyo zitakufa moja kwa moja na hazitaweza kusambaza tena virusi,” anasema.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya ya Israeli ilitangaza kwa mara ya kwanza kugawa dawa zenye uwezo wa kuzuia maambukizi kwa makundi yenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya. Dawa hizo zinazojulikana kama prophylactic drugs zinapomezwa mara kwa mara zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi.

Kwa sasa, dawa pekee kwa watu wenye virusi vya ukimwi, ni dawa za kupunguza makali ambazo humezwa kila siku ambazo pia hupunguza uwezekano wa maambukizi mapya.

Historia inaonyesha kuwa VVU ilitokea kwa nyani waliopo katika Afrika ya kati katika miaka ya 1900. Kutokana na mwingiliano kati ya tamaduni tofauti na mataifa, vilianza kusambaa duniani.

Ukimwi uligundulika nchini Marekani miaka ya 1980 na ulijulikana kama Ukosefu wa Kinga kwa Mashoga (GRID). Kadiri muda ulivyokwenda, wagonjwa wengine watano waligundulika nchini humo, wote wakiwa ni mashoga mwaka 1981.

Wakati watafiti na wanasayansi wakiendelea kuumiza vichwa kupata majibu ya dawa ya ugonjwa huu unaendelea kugharimu maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kila mwaka, bado tiba au kinga yake ya uhakika imekuwa mtihani mkubwa ambao hadi sasa hakuna aliyeufaulu. Hata hivyo, wugunduzi huu wa wanasayansi wa Israeli unaweza kubadilisha matokeo.

Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini zina asilimia ndogo mno ya maambukizi yanayokadiriwa kuwa 0.1. Hii ni tofauti na nchi za Kiafrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo karibu asilimia tano ya watu wake wanakadiriwa kuwa wameaambukizwa VVU.

Kwa sasa tuna watu 7,500 ambao wanaishi na VVU hapa Israeli,” anasema Dk. Margalit Lorber ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Afya cha Haifa's Rambam kinachoshughulika na magonjwa yanayotokana na upungufu wa kinga ya mwili. Wagonjwa wapya 450 huripotiwa kila mwaka,” anaeleza.

Wakati asilimia ya watu walioathirika na VVU nchini Israel ikiwa ni asilimia 0.1, nchi hiyo ilianza tafiti kuhusiana na ugonjwa huo miaka 1990 wakati kulipokuwa na msukumo mkubwa duniani juu ya utafiti wa VVU na Ukimwi.

Wanasansi walioshiriki katika utafiti wa dawa hiyo mpya wanasema, majaribio ya ufanisi wa dawa hiyo yataanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na wanatarajia kuifanya tiba hiyo kuwa ya gharama nafuu kuliko dawa zozote za ugonjwa huo.

Gammora: The Possible Israeli Cure for AIDS - The Media Line
Source jamiiforum

Saturday, March 11, 2017

Thursday, March 9, 2017

Friday, March 3, 2017

Dogo janja anunua gari jipya baada ya kuibiwa vifaa vya gari yake ya mwanzo tizama kwa taarifa zaidi#johnleo


Dogo Janja ameonesha jeuri ya fedha. Baada ya kuibiwa baadhi ya vitu kwenye gari lake aina ya Porte rapper huyo amenunua gari jingine jipya.
Gari hilo la sasa ambalo atakuwa anamiliki Dogo janja ni Raum new model yenye rangi nyekundu. Kupitia mtanda wa Instagram, Madee ameweka picha ya Janja akiwa juu ya gari hilo na kuandika, “Janjaro new car!!! Raum new model!!!.”
Wakati huo huo kuthibitisha kuwa jambo hilo halina utani, hitmaker huyo wa Kidebe ameweka picha hiyo hapo juu kwenye Instagram na kuandika, “Don mess up with BUDABOSS!🔥 ayah umeona dogo @youngkillermsodokii endelea kufuga icho kitoroli chako cha milion mbili

Thursday, March 2, 2017