Friday, December 15, 2017

Raid Magufuli: wanaosema vyuma vimekaza waweke gilisi#johnleo


Rais John Magufuli amesema vyuma vikikaza vinatakiwa kuwekwa grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa.

Amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Rais Magufuli amesema waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali ndiyo wanaosema vyuma vimekaza.

“Vyuma vimekaza na bado vitavunjika kabisa nawashauri muweke grisi,” amesema.

Msemo wa vyuma vimekaza umekuwa maarufu katika siku za karibuni ukiwa na maana maisha yamekuwa magumu.

Rais Magufuli amesema alipoingia madarakani alikuta changamoto nyingi zikiwemo za wafanyakazi hewa, vyeti feki na ufisadi. 

Amesema baada ya kudhibiti, watumishi wa umma 12,000 wamepatikana na vyeti feki wakiwemo walimu 3,655 tangu walipoanza kuhakiki.

Amesema uhakiki huo ulibaini watumishi hewa 20,000 na kwamba, Serikali ilikuwa inapoteza fedha nyingi kuwalipa mishahara.

“Kila kitu kilikuwa hewa hata mapenzi inawezekana yalikuwa hewa,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kutokana na udhibiti wa fedha za Serikali ni lazima watu waliokuwa wanapata fedha kwa njia zisizo halali watalalamika kuwa vyuma vimekaza.

Kuhusu madai ya walimu, amesema Sh25 bilioni wanazoidai Serikali zitalipwa baada ya uhakiki kumalizika

==>Msikilize hapo chini==>>

Majina ya wanajeshi waliopoteza uhai huko congo,#johnleo



Haya ni majina ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani.

Wanajeshi hayo ni;  
1.                    Hamad Haji Bakari, 
2.                  Chazil Khatibu Nandonde, 
3.                  Idd Abdallah Ally, 
4.                 Juma Mossi Ally,  
5.                  Ally  Haji Ussi, 
6.                 Pascal Singo, 
7.                  Samwel Chenga, 
8.                  Deogratius Kamili, 
9.                 Mwichumu Vuai Mohamed, 
10.              Hassan Makame, 
11.                 Issa Mussa Juma, 
12.               Hamad Mzee Kamna, 
13.               Salehe Mahembano na 
14.               Nazoro Haji Bakari.
Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.

Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.

Wednesday, December 13, 2017

Maelezo mafupi kuhusu blog ya johnleo inayomilikiwa na johnleo#johnleo

Naitwa john Marco ni kijana mjasiliamali nimezaliwa Tanzania mkoa wa simiyu katika wilaya ya bariadi kijiji cha old maswa kila mtu amezaliwa na kipaji chake na pia ana ndoto yake nina kipaji na pia Nina ndoto, kwa sasa tayari nina blog yangu ambayo huwa nafanya post za aina mbalimbali natamani siku moja nije kuwa na blog kubwa kama ya millardayo au michuzi blog na kadri mda unavoenda nitakuwa nabadilisha mwonekano was blog yangu jina la blog inaitwa johnleo.blogsport.com ukiitaji zaidi unanitafuta kupitia Facebook ambapo unaweza kuzipata moja kwa moja pia unaweza kunitafuta kupitia www.sindano.com ninachohitaji kwenu ni sapoti yenu mwezi ujao nitakuwa na account ya YouTube ambayo nitakuwa naweka huko pia kwa jina hilohilo la johnleo. By johnleo

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo December 14 2017 Udaku, Michezo na Hardnews#johnleo

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo December 14 2017 Udaku, Michezo na Hardnews

Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania December 14 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa


Rais Magufuli: Amuagiza Waziri wa Fedha kuhakikisha malipo kwa kutumia fedha za kigeni yanadhibitiwa.johnleo

Habari zenu wakuu

Benki ya CRDB inafungua tawi lake jipya mjini Dodoma katika Jengo la LAPF.

Tukio hili liko live TBC1.

Pamoja na wageni wengne yupo Mh. John Pombe Magufuli ambaye ni mgeni rasmi, katibu mkuu wizara ya fedha, mawaziri, spika wa bunge, mkurugenzi wa CRDB DR. Charles kimei na wageni wengne mbalimbali.

Kwa mujibu wa mh. Rais yeye ni miongoni mwa wateja wa CRDB na anaamini CRDB ina mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda na kutoa ajira kwa watanzania.

=======
Rais Magufuli: Amuagiza Waziri wa Fedha kuhakikisha malipo kwa kutumia fedha za kigeni yanadhibitiwa.

> Asema alizuia Mkataba ulioandaliwa na Benki Kuu uliopanga kulipa kwa Dola za Kimarekani. Asisitiza suala hili likiendelea Wasimlaumu.

Rais Magufuli: Pale Benki Kuu(BOT) kuna watu 17 wenye PhD lakini waliruhusu Benki moja kufanya biashara hapa nchini bila kutambua kuwa ni ya kibababishaji.

> Ilipozuiwa Marekani na wao ndio wakashtuka.

Rais Magufuli: Mabeki ambayo hayafanyi vizuri BoT isisite kuyafungia na kuacha mambo ya kubebana bebana

> Ni bora kubaki na beki 5 zinazofanya vizuri kuliko kuwa na benki nyingi zisizo na tija

Rais Magufuli: Najua Makao Makuu yenu yapo Dar lakini nitoa wito kwenu CRDB muangalie utaratibu wa kujenga Makao Makuu hapa Dodoma

> Kwanza itasaidia kutangaza benki yenu na hata mkiwa na jambo mtasaidiwa haraka kwa sababu hata Makao Makuu ya Serikali yatakuwa hapa

Saturday, December 9, 2017

Baada ya JPJ Magufuli kuwasamehe babu Seya na familia yake wasanii waguswa na kuandika haya#johnleo

Siku ya December 9, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa Familia ya Babu Seya, msamaha huo ameutoa wakati wa Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara Mjini Dodoma wakati akihutubia.
Baada ya msamaha huo wa Rais baadhi ya mastaa wameonesha kuguswa na msamaha huo ambapo wameamua kuandika kupitia kurasa zao za Instagram…na baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Mchekeshaji Katarina Karatu, Dkt. Cheni, Mh Temba, na Petit Man Wakuache, Afande Sele…
“Mungu ni mwema #salutejpm – Mh. Temba
“Hao uraian Asanteee Rais wangu Mzalendo wewe ndiye Jembe letu mh John Pombe Magufuli Barikiwa sana” – Dkt. Cheni
“Uhuru day pino babaaaaa JPM Tishaaaaa mzee baba” – Petitman Wakuachetz
“Saba mara sabini….Kongole mr president Jpm” – Afande Sele
BREAKING: JPM ameagiza kuachiwa huru kwa Babu Seya na Familia yake

Hatimae Rais John Pombe Magufuli leo aiachia huru familia ya babu Sega kuanzia leo wapo huru#johnleo

seya1.jpg
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza

Yametimia katika sherehe za Uhuru 2017. Katiba ya JMT Ibara ya 45 yatumika.
Karibuni kwa maoni na povu.

Rais John Magufuli akiwa kwenye kilele cha miaka 56 ya Uhuru amesemehe wafungwa waliohukumiwa kwa vifungo mbalimbali na kunyongwa.

Miongoni mwa waliosamehewa ni wanamuziki Nguza Viking Alias maarufu Kama Babu Seya na Johnson Nguza(Papii Kocha) ambao walihukumiwa kifungo Cha maisha gerezeni kwa kosa la kubaka na kulawiti watoto 10 mwaka 2003 na kuhukumiwa Juni 25, 2004.

Pia Rais Magufuli amemsamehe mzee Matonya mwenye miaka 85 ambae alihukumiwa kunyongwa na ameshakaa miaka 37 baada ya hukumu na miaka Saba mahabusu.

Friday, December 8, 2017

Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira atangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Johnleo

Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira atangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema ameridhika na mwenendo mpya wa Chama hicho chini ya Mwenyekiti wake, Dkt. John Pombe Magufuli na aimeiona CCM inayobadilika, na kuona juhudi za kila mtu, ameiona CCM inayoanza kukataa rushwa, na itaipeleka taifa mbele.

Amejiunga leo kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT) unaofanyika mjini Dodoma.

Saturday, November 25, 2017

Dr. Lous Shika amefunguka na kusema kwamba amefurahi sana baada ya kusikia kwamba Nyumba za Lugumi ambazoz jana zilifanyiwa mnada wa Marudio zimekosa mnunuzi.#johnleo

 


Dr. Lous Shika amefunguka na kusema kwamba amefurahi sana baada ya kusikia kwamba Nyumba za Lugumi ambazoz jana zilifanyiwa mnada wa Marudio zimekosa mnunuzi.

Dr. Shika ambae alikuwa mshindi wa kuzinunua nyumba hizo kwenye mnada wa awali lakini alishindwa kukamilisha mashrti ya mnada ya kulipa asilimia 25 ya fedha za manunuzi na kusababisha mnada huo kurudiwa tena jana amesema, kukosekana kwa mnunuzi kwenye mnada huo wa marudio imempa nguvu na kusema kwamba ndani ya wiki mbili atafanya mpango wa kuzilipia nyumba hizo.

"baada ya kusikia kwamba nyumba ambazo nimekuwa nikizihitaji kwa muda mrefu kwamba hazijanunuliwa hata mnada wa leo(jana),hiyo mimi imenipa nguvu,nimefurahi"

"Changu ni changu,basi katika wiki mbili hizi zinazofuata   hela itakuwa imeshaingia.Kumbe Mungu amenizunguka bado, yupo pamoja na mimi" .Alisema Dr.Shika


Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia#johnleo


Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia

Rais John Magufuli amesema hakubomoa jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopo Ubungo alipokuwa waziri wa ujenzi kwa kuwa aliogopa kufukuzwa kazi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumamosi Novemba 25,2017 alipozindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza mbele ya waziri mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mizengo Pinda aliyehudhuria uzinduzi huo, Magufuli amesema wakati huo aliogopa baada ya kuzuiwa na waziri mkuu huyo, lakini sasa yeye ndiye Rais hakuna wa kumzuia.

Akizungumzia ubomoaji unaoendelea sasa amesema, “Nilishatoa maagizo, najua Mizengo Pinda kwenye hili alinipinga wakati ule, lakini najua leo hawezi akanipinga kwa sababu mimi ndiye Rais. Wakati ule nilikuwa waziri wake, ndiyo maana nilinyamaza nilijua ninaweza nikafukuzwa, hutakiwi kumpinga mkubwa.”

“Hilo jengo la Tanesco, narudia kama itakuwa ni kubomoa nusu, no problem (hakuna tatizo); kama ni lote hakuna tatizo, pamoja na jengo la wizara ya maji. Najua katibu mkuu wa wizara ya maji yupo hapa ananiangalia, wakaanze kulitoa eneo lililopo kwenye hifadhi ya barabara,” amesema.

Machi 6, 2011 akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato, mkoani Kagera, Pinda ambaye alisifia utendaji wa Dk Magufuli alimwagiza kusimamisha ubomoaji maeneo kadhaa yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara likiwemo jengo la Tanesco hadi Serikali itakapotoa kauli nyingine kuhusu hilo.

Pinda alikuwa akizungumzia hatua ya Dk Magufuli aliyekuwa amewaagiza wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo na wasitarajie kulipwa fidia.

Pinda wakati huo akiwa waziri mkuu alisema spidi (kasi) ya Magufuli ilikuwa kubwa hivyo alimuagiza kusimamisha ubomoaji huo hadi suala hilo litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri.

Pinda, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia 2008 baada ya kujiuzulu kwa Edward Lowassa alisimamisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga upya.

Alisema Serikali inamuamini Magufuli kuwa kiongozi mwenye uwezo na ndio maana ilimpa nafasi akawabane makandarasi wazembe.

Dk Magufuli akiwasilisha bajeti bungeni mwaka 2012/13, alizungumzia ubomoaji akisema siasa iachwe akisisitiza sheria zimepitishwa ikiwamo Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na ya hifadhi ya barabara iliyoanza tangu mwaka 1932.

Alizungumzia jengo la Tanesco alisema liko kwenye hifadhi ya barabara na kwamba hata kama asipolibomoa yeye kuna siku litabomolewa vinginevyo sheria ibadilishwe.

Novemba 15 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Magufuli alimuagiza wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo la Tanesco na Wizara ya Maji, sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.
Chanzo: Mwananchi 

Saturday, November 18, 2017

Wednesday, August 9, 2017

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI#johnleo






TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.

Serikali inatarajia kuajiri Walimu 92 wa Shahada na 174 wa Stashahada wa masomo ya Fizikia, Hisabati, Kilimo na Biashara kwa Shule za Sekondari na Walimu 2,767 wa Cheti kwa Shule za Msingi.
Waombaji kwa shule za Sekondari wawe waliohitimu mafunzo ya Ualimu mwaka 2016 au kabla, na wale wa Shule za Msingi wawe waliohitimu mafunzo yao mwaka 2014 au kabla.
Sifa za Waombaji:
Walimu wa Sekondari:
Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo moja la kufundishia au zaidi au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo moja la kufundishia au zaidi pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali. Masomo ya kufundishia ni kati ya Fizikia, Hisabati, Kilimo au Biashara.
Stashahada ya Ualimu katika masomo yaliyoainishwa kwenye kipengele Na. 2.1 (i) hapo juu.
Cheti cha Kidato cha Sita
Cheti cha Kidato cha Nne
Walimu wa Shule za Msingi:
Astashahada ya Ualimu iliyotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Cheti cha Kidato cha Nne (wenye cheti Kidato cha Sita watapewa kipaumbele).
Utaratibu wa Kutuma Maombi:

Maombi yatumwe kupitia Posta kwa njia ya Rejesta (EMS).  Juu ya bahasha iandikwe kwa mkono "Maombi ya Kazi ya Ualimu - Sekondari au Maombi ya Kazi ya Ualimu - Msingi".
Mwombaji aambatishe nakala za Vyeti vilivyothibitishwa (Certified) na Mwanasheria pamoja na "Transcript".
NB:  Barua za maombi zisiwasilishwe kwa mkono.  Barua zitakazowasilishwa kwa mkono hazitapokelewa.

Masuala Mengine ya Kuzingatia:
Mwombaji aandike majina yake yote matatu.  Kama Vyeti vina majina mawili, utaratibu wa kisheria wa kuongeza jina uzingatiwe.
Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.
Mwisho wa kupokelewa maombi ni tarehe 31/08/2017.

Maombi yatumwe kwa:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.          

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA 

Saturday, July 1, 2017

Taarifa kwa uma kwa wahitimu wa stashahada wote tanzania#johnleo

TAARIFA KWA UMMA NA WAHITIMU WA STASHAHADA WOTE

BARAZA LA T
AIFA LA ELIMU YA UFUNDI(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSUWAHITIMU WA STASHAHADA KATIKAPROGRAMU MBALIMBALIWANAOKUSUDIA KUOMBAKUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YASHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YAJUU KWA MWAKA WA MASOMO2017/2018
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za usajili na ithibati, mitaala na upimaji ili tuzo zitolewazo na vyuo/taasisi ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. Kifungu cha 5 (1) (e) na (f) cha Sheria hii kinaipa mamlaka NACTE, kuanzisha tuzo mbalimbali zinazotolewa na kuhakikisha kuwa ubora wa elimu na mafunzo ya kada ya kati yatolewayo na taasisi mbalimbali yanazingatia ubora unaokusudiwa. Aidha, Kifungu cha 11, kinalitaka Baraza kuhakikisha kuwa Tuzo zitolewazo na vyuo na taasisi zote zinazoendesha mafunzo ya kada ya kati zinatambuliwa na mamlaka husika. Katika muktadha huu, kila chuo/taasisi inayotoa elimu ya ufundi inatakiwa kuwasilisha Baraza matokeo ya mitihani kila mwisho wa semista.
Hivyo, kwa kuwa Udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Shahada mbalimbali yanayotolewa na taasisi/vyuo vyote hapa nchini, utafanyikamoja kwa moja vyuoni, Baraza linao wajibu wa kuziwezesha taasisi/vyuo hivyo kudahili wanafunzi wenye sifa stahiki.
Ili kulifanikisha hili, Baraza limeandaa mfumo ambao taasisi/chuo kitapata taarifa za muombaji mwenye sifa linganifu (muhitimu wa Stashahada) moja kwa moja.
Hivyo, wahitimu wote wa Stashahada yoyote wanaokusudia kuomba kujiendeleza katika ngazi ya Shahada wanatakiwa kuhakiki taarifa zao Baraza (NACTE) kabla ya kufanya maombi yao kwenye taasisi/vyuo wanavyotaka kwenda kusoma. Uhakiki huo utafanywa kwa njia ya mtandao (online) kupitia Mfumo wa Uhakiki wa Tuzo(NACTE Award Verification System -NAVSkwa kubofyahapa au kupiti tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) kwa kubofya kitufe kilicho andikwa Award Verification. Baada ya kuhakiki taarifa zake kuwa kamilifu na sahihi, mhakiki atapatiwa Namba ya Utambulisho (Award Verification Number - AVN) ambayo itaambatanishwa na maombi ya Udahili kwenye taasisi/chuo husika. Utambulisho huo utatumiwa na taasisi/chuo kujiridhisha kwamba taarifa alizowasilisha muombaji wa Udahili ni sahihi na hivyo kuweza kudahiliwa na kisha kuchaguliwa kwa ajili ya masomo kulingana na mahitaji ya taasisi/chuo husika.
Aidha, Baraza linapenda pia kuwafahamisha wale wote walio na Stashahada walizopata nje ya nchi(Foreign Diploma Awards), nao waziwasilishe kupitia mfumo huu (NAVS) kwa ajili ya kuzifanyia ulinganifu na kuweka taarifa zao kwenye Kanzidata ya Baraza ili nao waweze kupata Namba ya Utambulisho. Maelezo ya namna ya kuziwasilisha tuzo za kufanyiwa ulinganifu yanapatika kwenye tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).
Ili mwombaji Udahili apate Namba ya Utambulisho atalipa Shilingi Elfu Kumi (10,000/=) kwa njia ya mtandao (Online) kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye Mfumo wa Uhakiki wa Tuzo -NAVS.  Kwa wale wanaotaka kufanya ulinganifu wa vyeti vyao, watatakiwa kulipa Shilingi Elfu Ishirini (20,000/=) kwa tuzo za ndani ambazo hazisimamiwi na baraza, na Shilingi Elfu Hamsini (50,000/=) kwa tuzo za nje ya nchi (foreign awards).
Baraza linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa wanaweza kufanya uhakiki huo kuanzia leo tarehe 28 Juni, 2017 hadi tarehe 20 Julai, 2017.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI(NACTE)
TAREHE: 28/06/2017