KARIBU SANA MSOMAJI WA MAKALA MBALIMBALI KATIKA BLOG YETU(MTEGA BLOG)
MATUMIZI YA BLOG
1.KUWEKA HABARI NA TAARIFA MBALAMBALI.
Unaweza
kutumia blog yako kuweka au kutangaza habari mbalimbali za
kikanda,kitaifa au hata za kimataifa.Habari kwa maandishi,Habari kwa
Picha na Habari kwa Sauti na Habari kwa Video,Chaguo ni lako.
2.KUWEKA TAARIFA ZAKO BINAFSI
Unaweza
kutumia BLOG kutunzia taarifa zako mbalambali kama vile matukia\o yako
ya kila siku,taarifa zako za nyumbani n.k ANGALIZO:KAMA UNATAKA UWEKE
TAARIFA ZA SIRI IWEKE BLOG YAKO KATIKA PRIVATE,Baada ya kufanya hivyo
hakuna mtu yeyote atakayeweza kuona taarifa zako hata kama akaingia
katika BLOG YAKO.
3.Kutangaza biashara yako
NDIO,
Kama una biashara yako na unataka kuinadi kupitia blog basi inawezekana
kabisa hapa kuna mbinu zinazohitajika ili uweze kufanikiwa katika
hili.Lugha ya Mvuto,Utumiaji mzuri wa Picha,kuwa Mbunifu na jifunze
jinsi ya kuongea na wateja.Toa ofa na mengineyo.
4.KUTUMIA BLOG KWA AJILI YA MAWASILIANO KATIKA KAMPUNI
Kivipi,
unaweza kuitumia blog yako kwa ajili ya mawasiliano ya kampuni au
Shirika mara nyingi blog za aina hii huwa zinwekewa password hivyo Mtu
asiyehusika hawezi kuingia.Hata wewe unaweza kufanya pia.
5.Kutumia Blog katika Taasisi Mbalimbali
Unaweza
pia Kuitumia Blog katika taasisi mbalimbali kama vile
Shule,Vyuo,Taasisi za kidini na hata Vikundi mbalimbali.Blog itasaidia
kurahisisha Mawasiliano.Kwa mfano Blog ya Shule inaweza KUTUMIKA kuweka
taarifa mbalimbali na matukio ya Shule/Chuo kama vile Ratiba ya
Vikao,Ratiba za Mitihani na mengineyo.Blog ya shule na Chuo pia inaweza
kutumika kuweka JOINING INSTRUCTIONS(Hii ni barua inayotoa mwongozo wa
MAELEKEZO Y KUJIUNGA NA CHUO AU SHULE HUSIKA) Kumekuwa na ugumu wa
kupatikana kwa barua hizi na hivyo kuwafanya wanafunzi MUDA MWINGINE,
kusafiri umbali mrefu kwenda shuleChuo kuchukua JOINING INSTRUCTIONS
LETTER,BLOG INAMALIZA TATIZO HILI.
TUNAKUTENGENEZEA BLOG KWA GHARAMA NAFUU KUANZIA TZS 20,000/= TU.
TUPIGIE 0758297744.
ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUJIINGIZIA KIPATO KWA KUPITIA BLOG.
Hii
ni sehemu muhimu ambayo karibu kila anayefungua blog anataka afahamu
jinsi gani anaweza kuingiza kipato kwa kupitia blog.Swali linakuja je ni
kweli mtu unaweza ukaingiza fedha kwa kupitia blog? Jibu ni NDIO
unaweza kuingiza kipato kwa kupitia blog.Kabla ya yote unatakiwa
ufahamu kuwa fedha ni thamani na thamani yoyote haipatikani pasipo
kuifanyia kazi,hivyo kuingiza fedha kupitia blog vivo hivyo inahitaji
ujitoe kwa kweli.Fahamu pia kuwa inahitaji muda hadi uweze kuingiza
kipato kupitia blog.Urefu wa muda unatofautiana kuna ambao wanaanza
kjiingizia kipato ndani ya siku kadhaa wengine miezi kadhaa na wengine
inafikia hadi mwaka au zaidi.Yote haya hutegemea Aina ya BLOG
na makala zinazowekwa,Kwa mfano ni vigumu kuingiza fedha haraka kama
utafungua blog ya ktoa taarifa na habari.Hata hivyo ukiwa Mbunifu zaidi
hakutakuwa na kikwazo.
1.KUWEKA MATANGAZO YA WATU KISHA WAKAKULIPA
Hii
ni njia namba moja na maarufu sana utakayoweza kuitumia kujiingizia
kipato kupitia blog yako.Fahamu kuwa kuna wafanyabiashara ambao
wanatafuta wateja mtandaoni.Ili uweze kumshawishi mtu aweke tangazo lake
katika blog yako lazima blog yako iwe na vitu vifuatavyo:
i)Lazima blog yako iwe na watembeleaji wengi.
i)Lazima
blog yako iwe hai(hii ina maana ya kwamba blog yako iwe inawekwa makala
mara kwa mara,isiwe umeweka makala leo,kisha unakaa mwezi mzima
haujaweka makala).
2.Kuifanya blog yako iwe ya kulipia
Hii
ni njia ya pili unayoweza kuitumia kujiingizia kipato kupitia.Faida
kubwa iliyopo ni kwamba wewe ndiye unaamua nani atazame blog
yako.Unaweza ukaifunga blog yako na ikawa hakuna mtu anayeweza kuingia
katika blog yako bila ya wewe kumruhusu.Na utamruhusu pale atakapofanya
malipo.
KUMBUKA:Ili
kuweza kutumia njia hii na uweze kufanikiwa katika kujiingizia kipato
kupitia blog yako ni lazima uandike vitu vya thamani,yaani uandike vitu
ambavyo vina faida kwa watu,pia viwe vitu ambavyo havipatikani sehemu
nyingine yoyote bure.Usihofu sio kazi kubwa unachotakiwa kufanya ni
kujifunza sifa au stadi za blogger aliyebobea.
Blogger=Mtu anayemiliki blog au anayeandika makala katika blog au mwendeshaji wa blog.
Jifunze jinsi ya kuwa Blogger aliyebobea(Mtaalamu).
Zifuatazo
ni sifa za Blogger aliyebobea(Unatakiwa uwe nazo sifa hizi ili uweze
kujiingizia kipato kupitia Blog).Usijali sio lazima zote,Anza na chache
Nyingine Utajifunza Baadae.
i/.Uwezo wa kuandika makala zenye mvuto na zinazoeleweka.
ii/.Uwezo wa kufanya tafiti,Blogger anatakiwa awe na uwezo wa kufanya utafiti juu ya yale anayotaka kuandika.
iii/.Blogger anatakiwa awe na uzoefu na Mitandao tafutaji(Search Engines) .
.Blogger anatakiwa awe na ujuzi wa kuandika kiufasaha.Andika kitu kinachoeleweka.
iv/.Kuwa na Nidhamu katika Blog yako.Weka Makala lkatika blog yako kwa Utaratibu Maalumu.
v/.Ujuzi katika matumizi sahihi ya picha namichoro.Picha na michoro ina umuhimu Mkubwa katika ka kuonngeza mvuto wa Makala.
.
3.Kuweka matangazo ya Google ADsense/Adword.
Unaweza
kuweka Matangazo kutoka Google /Wordpress na Ukalipwa kutokana na idadi
ya watembeleaji wa blog yako watakaotembelea Blog hiyo.Kuna sifa za
kuweza kuruhusiwa kuweka Matangazo ya Google au WordPress.
Hii pia inahitaji blog yako iwe na makala za kutosha na iwe na watembeleaji wakutosha.
4.Kutoa kozi mbalimbali ambazo watu watakuwa tayari kujiunga nakozi hizo NA KUZISOMA KWA MALIPO UTAKAYOWATOZA.Hii
wala si kazi kubwa ingawa inahitaji muda na kujitoa.Kama una ujuzi
wowote na unataka kuwafikishia watu kisha wakulipe basi fahamu kuwa
kupitia blog unaweza kuwafikia watu wengi sana utaifanikisha kazi hii
kupitia blog yako.Nakushauri kutumia Kiswahili kwani ndiyo lugha ambayo
watanzania wengi wana umahiri nayo kuliko lugha nyingine.
Ili uweze kufanikisha hili unatakiwa uweke ulinzi(wa password) KATIKA KOZI ZAKO.
5.Kutangaza biashara zako.
Tukiacha
kutangaza biashara za watu pia wewe mwenyewe unaweza kutangaza biashara
zako na ukaongeza wateja kupitia blog yako.Hii inajumuisha bidhaa zote
za mtandaoni na zisizo za mtandaoni.Unaweza kuandika vitabu mbalimbali
kuanzia vya masomo hadi vya hadithi na kadhalika.Vitabu hivi utaviandika
kupitia MS Word au program nyingine inayoweza kufanya huduma hiyo na
utawauzia wateja kwa kuwatumia katika email zao.
Ili
uweze kupata soko la uaminifu unaweza ukaandika kitabu cha kwanza na
kukitoa BURE KABISA au kwa Ofa.Usishangae, kufanya hivi kutajenga
uaminifu mkubwa na kama kitabu chako kitakuwa kizuri basi unaweza kupata
soko kubwa kwa vitabu utakavyovitunga baadae na kuviuza.
KUONGEZA WATEMBELEAJI KATIKA BLOG YAKO
1.Itangaze Blog yako katika Mitandao ya kijamii,kama vile Facebook,Twitter,Instagram,WhatsApp na kadhalika.
2.Andika makala zenye mvuto na zinazoeleweka.Hii itawafanya watembeleaji wawe wanatembelea mara kwa mara.
3.Itangaze blog yako kwenye mitandao mikubwa yenye watembeleaji wengi.
4.Kuwa
na utaratibu wa kukomment katika mitandao mikubwa yenye watembeleaji
wengi.kisha acha link ya blog yako,kwa njia hii unaweza kupata
watembeleaji,ila jitahidi kukomment kitu chenye maana/thamani.
5.Chukua
maoni ya wasomaji wako na uyafanyie kazi,hii itawafanya wasomaji wako
waendelee kutembelea blog yako kwani watakuwa wanakipata
wanachokitaka.Ukienda kinyume na wasomaji wako ,wanaweza kukukimbia na
kutafuta blog nyingine itakayowafaa.
6.Weka makala katika blog yako kwa utaratibu maalumu.
7.Andika
makala za muda mrefu.Makala za muda mrefu zina manufaa makubwa kwani
hatakama makala uliiandika mwaka uliopita bado itakuwa na thamani.Na
watu wataendelea kuisoma kwani bado ujumbe unatumika.Makala za habari
zinadumu kwa muda mfupi sana.
8.Kuwa
mbunifu ifanye blog yako iwe ya kuvutia,Buni Mwonekano wa blog yako uwe
wa kuvutia,kuna rangi nyingine Ukiweka unafukuza watembeleaji(Color
Psychology).
9.Kichwa cha makala kinachovutia.
Jitahidi kuandika kighwa cha makala kinachovutia ili umshawishi MSOMAJI Kuendelea kusoma.
10.Watambue wasomaji wa Blog yako.
Ni vema uwe na wasomaji 10 wa blog yako unaowatambua,kuliko kuwa na wasomaji 100 usiowatambua.
Ninapozungumzia
kufanikiwa kupitia BLOG yako wengi wanweza wakapeleka mawazo yao katika
UCHUMI,HASHA sina maaan hiyo,bali ninachikusudia hapa ni jinsi gani
unaweza kufanikiwa katika blog yako.Hii ni kwa sababu watu walio wengi
hawadumu katika blog zao ,yaani mtu akifungua blog baada ya muda mfupi
tu miezi kadhaa(na wengine hata siku kadhaa) HIVYO mtu wa aina hii
ameshindwa kufanikiwa katika blog yake.
Zifuatzo ni sababu zinazowafanya Watu wengi washindwe kufanikiwa kupitia blog zao.
1.Kiwewe cha BLOG.
Nini
maana ya kiwewe cha blog? Kiwewe cha Blog ni hali ya mtu kutamani sana
awe na(amiliki) blog,na kufikiria kuwa ni kazi rahisi sana,Ukweli ni
kwamba KUTENGENEZA BLOG ni kazi rahisi sana,tatizo linakuja katika jinsi
ya kuiendesha.Inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana la sivyo safari
yako ya blog itaishia njiani.Sababu hii huwafanya wengi waachilie mbali
kuhusu blog na hivyo kushindwa kufikia malengo.
2.UTIAJI Chumvi wa baadhi ya watu katika Matangazo yaao ya kujinadi.
Kuna
baadhi ya watu wanatia chumvi sana kiasi kwamba inaonekana kuwa
kutengeneza/kujiingizia fedha kupitia blog ni kama kazi ya saa moja
tu.Mfano unaweza ukakuta tangazo linalosomeka ‘’FUNGUA BLOG LEO UANZE
KUPOKEA FEDHA’’ au “FUNGUA BLOG LEO UANZE KUINGIZA KIPATO CHA MAANA,SI
AJABU WENGINE WANAFIKIA HATA KUSEMA UWE TAJIRI’’.Matangazo ya namna hii
na kwa mtu mwenye uelewa wa chini anayachukulia kama yalivyo.Pia
wanashindwa kufahamu kuwa hiyo ni Lugha ya kibiashara tu.SI UONGO BLOG
inaweza kukufikisha KWENYE UTAJIRI Lakini si kwa haraka na kiurahisi
namna hiyo.Watu wa namna hii mara nyingi huishia kufunguia blog tu na
kuiacha kwani anakuta mambo tofauti na vile alivyoambiwa.
3.KUKOSA CHA KUANDIKA
Wapo wanaoshindwa kupata cha Kuandika,na hivyo huishia kati katika safari yao ya Blog.
>>>SULUHISHO:Hakuna
kitu kipya Duniani usiogope kuona hakuna kipya,utakachoandika kwa kuona
kila kitu kimeshaandikwa.Andika tofauti na Wenzako,kuwa Mbunifu na hii
ndio faida ya kufanya utafiti kwani utafahamu mapungufu ya wengine
katika makala zao na utajua jinsi gani utayarekebisha kupitia makala
zako mpya utakazoandika.
PIA,Jijengee
utaratibu wa kujisomea Soma Vitu Mbalimbali vitakavyokuongezea
Maarifa.Soma mtandaoni,soma vitabu,soma magazeti n.k.Ukijijengea
utaratibu wa kujisomea utaongeza maarifa ya kutosha yatakayokuwezesha
kupata makala za kuandika,sio kucopy.
4.KUTOKUWA WAVUMILIVU
Kuifanya
Blog yako iwe chanzo cha mapato inahitaji Muda wa kutosha.Sio rahisi
kuanza kufungua Blog leo na kesho ukaanza kupokea fedha.Kutokana na hali
hii watu wasiokuwa wavumilivu huamua kuachana na Blog.
>>>SULUHISHO:Inahitaji kuwa Mvumilivu ili uweze kufanikiwa katika blog yako.Kuwa Mvumilivu na tumia mbinu mbalimbali kuiboresha blog yako.
5.KUTOPATA WATEMBELEAJI
Kupata
Watembeleaji katika Blog yako inategemea vitu vingi.Kuna watu
wanapofungua blog na kuona hakuna watembeleaji huamua kuachana na blog.
>>>>SULUHISHO:Ili kuongeza Watembeleaji katika blog yako Tumia mbinu zifuatazo.
*UNAHITAJI USHAURI KUHUSU BLOG YAKO TUANDIKIE(BURE!!)
E-Mail:godfreymtega@gmail.com
"TUTAKUTENGENEZEA APPLICATION YA ANDROID YA BLOG YAKO"
TUNAKUTENGENEZEA BLOG KWA GHARAMA NAFUU KUANZIA TZS 20,000/= TU
TUPIGIE :0758297744(whatsapp)/0716824009