Saturday, November 25, 2017

Dr. Lous Shika amefunguka na kusema kwamba amefurahi sana baada ya kusikia kwamba Nyumba za Lugumi ambazoz jana zilifanyiwa mnada wa Marudio zimekosa mnunuzi.#johnleo

 


Dr. Lous Shika amefunguka na kusema kwamba amefurahi sana baada ya kusikia kwamba Nyumba za Lugumi ambazoz jana zilifanyiwa mnada wa Marudio zimekosa mnunuzi.

Dr. Shika ambae alikuwa mshindi wa kuzinunua nyumba hizo kwenye mnada wa awali lakini alishindwa kukamilisha mashrti ya mnada ya kulipa asilimia 25 ya fedha za manunuzi na kusababisha mnada huo kurudiwa tena jana amesema, kukosekana kwa mnunuzi kwenye mnada huo wa marudio imempa nguvu na kusema kwamba ndani ya wiki mbili atafanya mpango wa kuzilipia nyumba hizo.

"baada ya kusikia kwamba nyumba ambazo nimekuwa nikizihitaji kwa muda mrefu kwamba hazijanunuliwa hata mnada wa leo(jana),hiyo mimi imenipa nguvu,nimefurahi"

"Changu ni changu,basi katika wiki mbili hizi zinazofuata   hela itakuwa imeshaingia.Kumbe Mungu amenizunguka bado, yupo pamoja na mimi" .Alisema Dr.Shika


Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia#johnleo


Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia

Rais John Magufuli amesema hakubomoa jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopo Ubungo alipokuwa waziri wa ujenzi kwa kuwa aliogopa kufukuzwa kazi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumamosi Novemba 25,2017 alipozindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza mbele ya waziri mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mizengo Pinda aliyehudhuria uzinduzi huo, Magufuli amesema wakati huo aliogopa baada ya kuzuiwa na waziri mkuu huyo, lakini sasa yeye ndiye Rais hakuna wa kumzuia.

Akizungumzia ubomoaji unaoendelea sasa amesema, “Nilishatoa maagizo, najua Mizengo Pinda kwenye hili alinipinga wakati ule, lakini najua leo hawezi akanipinga kwa sababu mimi ndiye Rais. Wakati ule nilikuwa waziri wake, ndiyo maana nilinyamaza nilijua ninaweza nikafukuzwa, hutakiwi kumpinga mkubwa.”

“Hilo jengo la Tanesco, narudia kama itakuwa ni kubomoa nusu, no problem (hakuna tatizo); kama ni lote hakuna tatizo, pamoja na jengo la wizara ya maji. Najua katibu mkuu wa wizara ya maji yupo hapa ananiangalia, wakaanze kulitoa eneo lililopo kwenye hifadhi ya barabara,” amesema.

Machi 6, 2011 akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato, mkoani Kagera, Pinda ambaye alisifia utendaji wa Dk Magufuli alimwagiza kusimamisha ubomoaji maeneo kadhaa yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara likiwemo jengo la Tanesco hadi Serikali itakapotoa kauli nyingine kuhusu hilo.

Pinda alikuwa akizungumzia hatua ya Dk Magufuli aliyekuwa amewaagiza wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo na wasitarajie kulipwa fidia.

Pinda wakati huo akiwa waziri mkuu alisema spidi (kasi) ya Magufuli ilikuwa kubwa hivyo alimuagiza kusimamisha ubomoaji huo hadi suala hilo litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri.

Pinda, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia 2008 baada ya kujiuzulu kwa Edward Lowassa alisimamisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga upya.

Alisema Serikali inamuamini Magufuli kuwa kiongozi mwenye uwezo na ndio maana ilimpa nafasi akawabane makandarasi wazembe.

Dk Magufuli akiwasilisha bajeti bungeni mwaka 2012/13, alizungumzia ubomoaji akisema siasa iachwe akisisitiza sheria zimepitishwa ikiwamo Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na ya hifadhi ya barabara iliyoanza tangu mwaka 1932.

Alizungumzia jengo la Tanesco alisema liko kwenye hifadhi ya barabara na kwamba hata kama asipolibomoa yeye kuna siku litabomolewa vinginevyo sheria ibadilishwe.

Novemba 15 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Magufuli alimuagiza wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo la Tanesco na Wizara ya Maji, sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.
Chanzo: Mwananchi 

Saturday, November 18, 2017